JUMLA ya Watoto 18,353 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya sindano ya surua na rubela  katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga

Akizindua zoezi hilo la utoaji wa chanjo  katika Kijiji cha Gezani kilichopo kata ya Manza wilayani humo Kaimu Mkurungenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Juma  Hamadi  amesema  zoezi hilo  ni sehemu ya muendelezo wa hamasa ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa walengwa.

“Naomba niwahamasishe wazazi na walezi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika vituo vyote vya afya, zahanati, na maeneo lengwa ili kuhakikisha kila mtoto anapatiwa chanjo hiyo ili kujikinga na magonjwa hayo ambayo ni hatari kwa afya zao, “amesema Hamadi.

Nae Mganga Mkuu  wa Halmashauri hiyo Dk Salvio Wekesi amesema  ugonjwa wa Surua na Rubella husababishwa na virusi vinavyoenea kwa njia ya hewa na kuleta madhara kwa watoto ambao hawajapata chanjo na wale wasiopata kinga kamilifu hivyo jamii inaendelea kupewa msisitizo wa kuhakikisha wanawapeleka watoto  kupatiwa chanjo hizo ili kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo

Share To:

Post A Comment: