MAMLAKA za Serikali za Mitaa zimeagizwa kutumia zaidi mfumo wa Ukusanyaji Mapato ( TAUSI ) ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi zinazoingia serikalini badala ya mifumo hiyo kuchezewa na kupelekea fedha kukaa kwa muda mrefu mikononi mwa watu wasio waaminifu.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha nne cha serikali mtandao(e-GA) cheye kuli mbiu ya Kuhakikisha uzingatiaji sera, sheria ,viwango na miongozo ya serikali mtandao kwa ubadilishanaji salama wa taarifa.

Amesema uchezeaji wa mifumo wa Tausi hupelekea fedha za kodi zinazopaswa kulipwa na wananchi kwenye mifumo kukaa kwa muda mrefu bila kulipwa na kupelekea baadhi ya watumishi kukaa nazo mikononi bila kukusanywa na kuwekwa katika mufumo sahihi ya serikali.

“Serikali imejenga mkongo wa Taifa na mifumo mingine muhimu lakini watu wanakwamisha mifumo hiyo na kukaa na fedha za serikali haswa kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa lazima muhakikishe mfumo wa Tausi unafanya kazi katika serikali za mitaa ili kodi za wananchi zilipwe kusema mfumo upo chini ni kuweka mazingira yasiyo rafiki ya rushwa na ufanyakaji kazi kwa ufasaha”

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mhandisi Benedict Ndomba amesema mamlaka hiyo imeunganisha taasisi za umma 109 na mifumo 117 imesajiliwa ikiwemo taasisi nne za haki jinai zikiwa zimeunganishwa na mfumo huo na kurahisisha utoaji huduma kwa haraka zaidi

Share To:

Post A Comment: