Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agness Marwa amekabidhi mitungi ya Gesi kwa kikundi kinachojishughulisha na upishi katika Kijiji cha Rwanga kata ya Rusoli Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

Akikabidhi mitungi hiyo Mbunge huyo amesema lengo la kutoa mitungi hiyo nikuhakikisha wanakimama wanaondokana na matumizi ya kuni.

“Lengo la serikali nikulinda Mazingira yetu kila mtu anawajibu wakuacha kukata ndio maana tunatoa mitungi ya Gesi kuhakikisha tunalinda misitu yetu”Alisema Agness Marwa Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mara

Baadhi ya akina mama ambao wamenufaika na msaada huo Wamemshukuru Mbunge Agness Marwa kwani sasa watafanya shughuli zao kwa urahisi na kuondokana na ukataji wa kuni kwani ilikuwa changamoto kubwa kwao.

Share To:

Post A Comment: