Na Samwel Mhadisa

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi leo Februari 8 2024 amewasili Nchini Kenya, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Baraza la kisekta la Mawaziri la bonde la Ziwa Victoria, akimuwakilisha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Mkutano huo, pia utapokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa program, miradi, maamuzi na maagizo mbalimbali katika sekta ya bonde la ziwa Victoria na masuala ya kiutawala katika kamisheni hiyo.

Aidha, Baraza hilo la Mawaziri la kisekta la Kamisheni ya bonde la Ziwa Victoria, linalojumisha Mawaziri wa Maji na Mawaziri wengine, pia watahusika na program na miradi inayotekelezwa na kutoa miongozo ya kisera kwa niaba ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo, pia utapitiaji taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria na taarifa ya Kamati za kikanda za Makatibu Wakuu, za uendeshaiji wa program na miradi ya kamisheni ya bonde hilo.

Katika safari hiyo ya Nchini Kenya, Mhandisi Mahundi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Dkt. George Lugomela pamoja na Robert Sunday

Share To:

Post A Comment: