wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UVCCM wakiongozwa na Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) wamefungua tawi la wakereketwa la Bodaboda lililopo Mahakama ya Zamani Babati Mjini ambapo alipata wasaa wa kusikiliza kero za maafisa usafirishaji (Bajaji na Bodaboda) na mawakala usafirishaji.
Kero zilizowasilishwa nyingi zilitatuliwa papo kwa hapo na nyingine Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi alimuelekeza Mkuu wa wilaya ya Babati Mjini kutatua kero hizo na Mkuu wa Wilaya alikiri kero hizo zipo ndani ya uwezo wake na atakaa na maafisa usafirishaji na kuweka mambo yote sawa ili maafisa usafirishaji na mawakala wa usafirishaji wafanye kazi yao bila usumbufu wowote.
Post A Comment: