Kamati ya kudumu ya Bunge Utawala , Katiba na Sheria imeipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kupeleka pesa katika miradi yenye tija kubwa ya Watu kupitia mfuko wa TASAF baada ya kukagua mradi wa Stendi ya Mabasi Peramiho na Soko la Bidhaa mbalimbali, Madaba.

Akizungumza mbele ya wananchi Mwenyekiti wa Kamati hiyo aliwashukuru sana serikali kwa miradi hiyo uku akieleza furaha ya Kamati baada ya kupitia miradi hiyo. 

Mapema akimkaribisha Mwenyekiti wa kamati, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ndg. Ridhiwani Kikwete alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 ambazo zimewezesha miradi mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma pekee kupitia TASAF.Share To:

ABDULLMAKAVELL

Post A Comment: