Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii cha kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi hiyo na Taasisi zake ya bajeti kwa kipindi cha Julai-Disemba, 2023 na Maazimio ya Bunge kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2023 Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia wasilisho la taarifa ya Ofisi hiyo wakati wa Kikao hicho.

Wakuu wa Taasisi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia wasilisho la Taarifa ya Bajeti ya Ofisi hiyo kwa kipindi cha Julai- Disemba, 2023 wakati wa kikao hicho

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imempongeza Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inakuwa na uhimilivu.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Fatuma Toufiq ameyasema hayo Januari 18, 2024 kwenye kikao cha kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha Julai-Desemba, 2023 na maazimio ya Bunge ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na taasisi zake.

Amesema kamati imeshuhudia jitihada za Rais kupitia Ofisi hiyo za kuimarisha mifuko ya PSSSF (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambayo imekuwa ikitoa mafao kwa wakati na kufanya uwekezaji wenye tija.

Pamoja na hayo, kamati imepongeza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa kuimarisha masuala ya usalama na afya na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa kuboresha utendaji kazi wake na kusimika kwa mfumo wa kielektroniki wa uendeshaji mashauri na utunzaji kumbukumbu katika ofisi zake zote.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako, ameahidi ofisi yake itaendelea kufanyia kazi ushauri wa kamati ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Share To:

Post A Comment: