Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa siku 10 kwa timu iliyoundwa na Ofisi ya RAis TAMISEMI kuchunguza ubora na thamani ya ujenzi Hospitali ya wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro baada ya makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa Hospitali hiyo.

Mhe. Dkt. Mpango alitoa maelekezo kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa ziara yake Machi 21,2024 alipofanya ziara wilayani hapo na kumtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI  kuunda timu ya kuchunguza thamani ya fedha na hatua za ujenzi wa Hospitali hiyo.

Kufuatia maelekezo Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amefika wilayani hapo akiwa ameongozana na timu hiyo na amekagua majengo yaliyojengwa kwa awamu ya kwanza kwa fedha iliyotolewa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na awamu ya pili kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambazo kwa awamu zote mbili ni Zaidi ya Bilioni 2.

“Nimejiridhisha Papi zilizokuwa zimewekwa na Top za milangoni zilizokuwa zimwekwa zimeondolewa baada ya makamu wa Rais kutilia shaka ubora wa milango hiyo na nimewahoji Engineer na msimamizi wa mradi wamekiri ni kweli zilikuwa hazina ubora  kwa hili Halmashauri ya Mwanga Haikuzingatia maelekezo ya serikali ndio maana mmejiridhisha mmeng’oa hiyo milango na katika muktadha huo lazima tuchukuwe hatua” amesema Dkt. Festo Dugange 

Aidha, Dkt. Dugange ameuelekeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kuhakikisha ifikapo Mei 10,2024 Hospitali ya wilaya hiyo iwe imeanza kutoa huduma kwa wananchi kwa huduma za wagonjwa nje OPD na Maabara

Kwa upande wake mkuu waWilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya amesema yeye na kamati ya ulinzi watatoa ushirikiano kwa timu hiyo na kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI huku akimshukuru Naibu Waziri kwa kufika na kukagua miradi ya Afya inayoendelea na ujenzi katika wilaya hiyo.





Share To:

Post A Comment: