Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imezindua rasmi zoezi la utoaji chanjo ya Surua ambapo watoto zaidi ya 18,624 walio chini ya miaka mitano wilayani humo wanatarajiwa kufikiwa na chanjo hiyo.

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amewataka wazazi kutopuuza elimu ya utoaji chanjo inayotolewa na watoa haduma ya afya kwani endapo watapuuza itapelekea watoto kukimbwa na madhara mbalimbali.

” Tuzingatie chanjo za watoto wetu katika hatua zao za ukuaji, moja ya mambo muhimu katika malezi ni kuhakikisha mtoto anapata chanjo kila anapohitajika kupatiwa”.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Sunday Deogratius amewapongeza wazazi waliojitokeza kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo na kuongeza kuwa sambamba na kupata chanjo lakini pia wazazi wanapaswa kuzingatia makundi matano ya vyakula ambayo humjenga mtoto na kuwa na afya bora.

Hata hivyo kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Stanley Mlay amesema lengo lao ni kuwafikia watoto wote walio chini ya miaka mitano hivyo zoezi hilo litafanyika katika vijiji vyote 77 vya wilaya hiyo.





Share To:

Post A Comment: