Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha maalumu ambazo amezielekeza kwenye mafunzo ya walimu wa elimu maalumu.

 

Dkt. Komba amebainisha hayo leo Januari 28, 2024 wakati akifungua mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kwa walimu wa Elimu maalumu kutoka halmashauri saba nchini, ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yaliyotolewa kwa maafisa elimu maalumu wa halmashauri hizo.

 

Amesema, katika mafunzo hayo walimu watapitishwa kwenye mbinu mbalimbali ikiwemo za kuongea, kuandika na kusoma zitazomsaidia mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu katika ujifunzaji.

 

Aidha, Dkt. Komba amesema, katika Mtaala huu ulioboreshwa masomo ya Sayansi ya kompyuta kama vile, kompyuta programing na coding yataa kutolewa kuanzia darasa la tatu, hivyo ni muhimu wanafunzi wetu wa elimu maalumu wakaweza kuyaelewa.

 

Sambamba na hilo, ametoa rai kwa walimu hao waliokuja kwenye mafunzo kufuatilia kwa umakini na weledi ili fedha hizo zilizotolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zioneshe tija kwa kumwezesha mwanafunzi mwenye uhitaji maalum kumudu mazingira yake baada ya kumaliza masomo na kupunguza utegemezi.

Share To:

Post A Comment: