Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) imekabidhi mbegu za ruzuku za Alizeti tani 55 pamoja na Ngano tani 40 tarehe 7 Machi 2024, katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Mkoani Arusha.

 

Akipokea mbegu hizo za ruzuku, Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Fred Lowassa amepongeza Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini kwa kupeleka kwa muda muafaka mbegu hizo kwa wakulima.

 

ASA inaendelea na zoezi la kusambaza mbegu za ruzuku za Ngano na Alizeti zinazotolewa na Serikali chini ya Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa kuwezesha upatikanaji wa pembejeo za kilimo Tanzania (Tanzania Agriculture Input Support Project -TAISP).

 

Shabaha ya Usambazaji wa mbegu chini ya mradi wa TAISP kwa mwaka 2023\/2024 ni tani 500 kwa Ngano na tani 700 kwa Alizeti.

Share To:

Post A Comment: