Shime yatolewa kwa Wananchi wote Nchini kutoa ushirikiano katika Tafiti za kitakwimu zinazoendelea Sasa za masuala ya utafiti wa Kilimo na masuala ya Uchumi.


Shime hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule Leo hii katika Mkutano wake na wanahabari wakati akitoa taarifa kuhusu Tafiti za kitakwimu zinazoendelea katika maeneo mengi Nchini na kuhamasisha wanachi kushiriki Tafiti hizo.

"Kumbukeni kadri mnaposhiriki katika tafiti kama hizi ndivyo Serikali inapogundua changamoto ambazo zinawakabili wananchi na hatimae kuchukua hatua stahiki. Hivyo, kushiriki tafiti kama hizi ni sehemu ya mchango wako mwananchi katika kuleta maendeleo ya mkoa wetu na maendeleo ya nchi nzima. Takwimu zinazotokana na tafiti hizi ni miongoni mwa vigezo vinavyotumika katika kugawa rasilimali za taifa, kufanya maamuzi katika kuongeza wigo wa utoaji huduma na kuimarisha ubora wake, ujenzi wa miundombinu na miradi mingine ya maendeleo. 
Kwa hiyo, shime wananchi tushirikiane kuyatekeleza haya. Kwa viongozi katika ngazi ya Wilaya, Kata, Vitongoji na Mitaa kwenye maeneo ya utafiti wajibu wetu ni kuhakikisha tunawapa ushirikiano wadadisi wataokafika katika maeneo yetu na kuwatambulisha kwa washiriki wa tafiti hizi. Sina shaka yoyote jukumu hili mnalielewa vyema na ni matumaini yangu kuwa mtalitekeleza kama mnavyofanya katika tafiti au majukumu mengine yanayofanana na haya".

Aidha Mh Senyamule amesema utafiti wa kilimo wa mwaka 2023/2024 utafanyika Tanzania nzima kwenye jumla ya maeneo 1352 Kati ya maeneo hayo 1234 ni ya Tanzania Bara na maeneo 118 ni ya Zanzibar.

"Utafiti huu ni muhimu sana kwa kuwa sekta ya kilimo inachangia wastani wa asilimia 26.2 ya pato la taifa, inatoa ajira kwa karibu asilimia 65 ya watu wote nchini, inatuhakikishia usalama wa chakula na ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya sekta nyingine husasuni sekta ya viwanda. Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2023/24 utafanyika Tanzania nzima kwenye jumla ya maeneo 1,352. Kati ya maeneo hayo 1,234 ni ya Tanzania Bara, na maeneo 118 ni ya Zanzibar. Jumla ya kaya za kilimo 16,224 zitahojiwa nchi nzima, kati ya hizi 14,808 ni za Tanzania Bara na 1,416 ni za Zanzibar. Utafiti huu utafanyika katika ngazi ya Kaya (kwa wakulima wa mashamba madogo) na katika ngazi ya Taasisi (kwa Mashamba Makubwa). [Katika mkoa wetu maeneo yaliyochaguliwa kufanyika Utafiti huu ni 61.

Sambamba na hayo pia amaelezea madhumuni ya utafiti huu ambapo amesema ni kupata idadi kamili ya Shughuli za kiuchumi na kilimo kwa ujumla.

"Madhumuni ya Utafiti huu ni kupata idadi ya shughuli za kiuchumi na kijamii zilizopo katika sekta iliyo rasmi Tanzania Bara; kupata muhimili wa sampuli (sampling frame) kwa ajili ya tafiti nyingine za kiuchumi na kijamii zitakazofanyika; na kutumika kama muongozo kwa watafiti mbalimbali. Taarifa zitakazokusanywa ni pamoja na jina la Shughuli, Eneo/Mahali ilipo, Anuani ya Posta, Namba ya Simu, Shughuli Kuu, Hali ya Umiliki, Mwaka wa Shughuli/Ofisi kuanza kufanya kazi, Mwezi na mwaka wa kusajiliwa shughuli au ofisi, Idadi ya Wafanyakazi kwa Jinsi na jumla ya Mapato kwa Mwaka. Aidha, taarifa hizi zinatumiaka kufanya uchambuzi wa kina wa kiuchumi kama kupima tija kwenye uzalishaji, kutathmini mwenendo wa uchumi na zitasaidia katika uundaji wa sera kwa kutumia taarifa sahihi na maamuzi sahihi. Utafiti huu unafanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa kipindi cha SIKU 60 na umeanza Tarehe 5 Novemba 2023".

Pia ameeleza kuwa taarifa zitakazo kusanywa katika utafiti wa kilimo wa mwaka 2022/2023 kuhusu orodha ya wanakaya,mashamba na vishamba na uzaishaji wa mazao kwenye mazao hayo.

"Katika Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2022/23 taarifa zinakazokusanywa ni kuhusu orodha ya wanakaya na taarifa zao za kidemografia, mashamba na vishamba, uzalishaji wa mazao kwenye mashamba hayo, upatikanaji wa mbegu na miche, matumizi na upatikanaji wa pembejeo (mbolea na viuatilifu), uzalishaji wa mifugo pamoja na mazao yake, utunzaji viumbe maji, kazi za ndani na nje ya kaya, na shughuli nyingine za kiuchumi. Utafiti huu utafanyika kwa muda miezi 2.5 kwa mashamba madogo na mwezi mmoja kwa mashamba makubwa. Kitakwimu mwaka wa kilimo unaanza tarehe 1 Oktoba ya mwaka uliopita hadi tarehe 30 Septemba katika mwaka wa utafiti. Hivyo kwa Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2022/23 taarifa zitakazokusanywa ni za tarehe 1 Oktoba 2022 hadi tarehe 30 Septemba mwaka 2023".

Naye mratibu wa Sensa Mkoa wa Dodoma Bwana Idd Muruke ameongeza kuwa utafiti huu ulikuwa ni kwa siku 60 ambapo uliaza November 5 2023 na walipaswa kumaliza January 5 lakini walipumzika kwaajili ya sikukuu kutoka December 24 mpaka January 5 hivyo ule utafiti wa mwezi Mmoja utaisha tarehe 19 na ule wa miezi miwili na nusu utaisha tarehe 28 January.

Utafiti huu wa kilimo na Uchumi ni wa siku 60 na utafanyika kote Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Share To:

Post A Comment: