Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Shirika hilo Upande wa Zanzibar Bw. Hillary Mwinyi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya 10 ya Kibiashara yaliyofanyika Uwanja wa Fumba Zanzibar.
Maonesho hayo ambayo ni sehemu ya shamrashamra ya Sherehe ya Miaka 60 ya Mapinduzi Bw. Mwinyi alisema TTCL imefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja nakuziunganisha nchi kadhaa ambazo zinapita katika Mkongo wa Taifa wa mawaisiliano ikiwa ni pamoja na Burundi, Malawi, Uganda na Congo.
Katika maonesho hayo TTCL iliweka miundombinu ya mawasiliano (Intaneti) katika eneo la uwanja wa Maonesho ambapo huduma hii iliwarahisishia na kuwawezesha washiriki wa maonesho hayo kupata huduma na kuwa nyenzo muhimu ya kufanikisha majukumu yako kwa kipindi chote cha maonesho.
Bw. Mwinyi alisema miaka 60 ya Mapinduzi shirika hilo limehakikisha mawasiliano yanaimarika ili kuendana na ukuaji na mahitaji ya teknolojia ya mawasiliano na hivyo kuwapa wananchi uwezo wa kuwasiliana kwa kasi na ubora.
TTCL imetumia fursa ya maonesho hayo ya 10 yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoa elimu ili kuwapa ufahamu Wananchi mbalimbali wanaofika katika Banda la shirika hilo kuhusu wajibu na kazi zinazofanywa na shirika hilo.
Alisema katika kipindi cha miaka 60 ya Mapinduzi TTCL inajivunia kurahisisha zaidi shughuli za kijamii na kiuchumi kutokana nakuviunganisha Visiwa vya Pemba na Unguja kwa njia ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo kuunganishwa kwa visiwa hivi ni moja ya mafanikio makubwa ya mapinduzi ya kiuchumi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwani imesaidia kupunguza gharama za mawasiliano kwa kiasi kikubwa.
Aidha alisema miaka 60 ya Mapinduzi TTCL imeleta ufanisi mkubwa katika utendaji wa shughuli za serikali hasa katika sekta ya Elimu, Afya, kilimo mtandao na kukidhi matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la matumizi ya Tehama kwa wananchi katika kuwapatia huduma kwa haraka zaidi.
Post A Comment: