Na Denis Chambi, Tanga.

MWENYEKITI wa Chama chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman amewaagiza viongozi wa serikali  na  wa chama ngazi ya kata kuweka utaratibu  wa kuwapima  mara kwa mara uja uzito  wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari ili kuweza kubaini waathirika na hatua kali za kisheria ziweze kuchukliwa.

Agizo hilo amelitoa  mara baada ya kufanya ziara katika kata ya Masaika wilaya ya Pangani mkoani Tanga ambapo alipata taarifa ya wanafunzi wawili wa shule ya msingi masaika waliopata ujauzito na lulazimika kufika nyumbani kwa mmoja wa wahanga hao ambapo wazazi wake walimweleza kuwa taarifa zilifika kwenye mamalaka za kisheria lakini mtuhumiwa aliachiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa hakukuwepo na ushahidi.

"Inasikitisha na inaumiza kwa kweli kuona mtoto anazaa mtoto,  na nyie viongozi wa chama mpo fuatilieni haya mambo kuisimamia serikali kuhakikisha watoto wetu hawa muda baada ya muda wanapimwa ili tujue wangapi ambao wapo salama na wangapi ambao wameathirika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na iwe fundisho kwa wengine" alisema Abdulrahman.

"Inasikitisha sana Rais wetu ametulete fedha kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemobsekta ya elimu lakini pia amefuta ada kuanzia darasa la kwanza mpaka sekondari lakini wapo watu ambao wanawapa vijana wetu mimba hii inasikitisha na  kuhuzunisha sana kuona bado kuna watoto wetu wanapata ujauzito niwaombe kila mzazi amuonee mtoto wa mwenzake uchungu huwezi jua mtoto huyu atakuwa nani baadaye niwaombe sana tuwalinde ,  tuwalee watoto wetu vizuri na tusiwafiche watoto tueni wakali kwa wale wenye nia mbaya ya kuwaharibu watoto wetu waweze kuchukuliwa hatua ili liwe fundisho kwa wengine"

Aidha amewataka viongozi kusimamia na kutekeleza wajibu wao ikiwemo kusimamia haki pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaovunja sheria huku akiwataka wananchi kiendelwa kudumisha amani kuelekea chaguzi za serikali za mitaa zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu 2024

"Kuna udhaifu wa kiuongzi kwa sababu kama serikali ya kijiji ingesimama imara ikashiriki katika jambo hili kuwakamata wahalifu naamini haki ingeweza kupatikana,  nyinyi kama viongozi  wajibu  wenu ni kuhakikisha kuwa mnawajibika kusimamia haki na inapatikana kwa sababu mtoto wa mwenzako ni mtoto wako ,  huu ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa niwaombe sana tuendeleze umoja na amani katika maeneo yetu chaguzi hizi zisitugawe" alisisitiza.

Akieleza bana mzazi wa mtoto huyo ambaye jina lake tumelihifadhi alieleza kuwa  alipata taarifa za mtoto wake kuwa ni mjamzito kutoka kwa walimu baada ya kuwapima wanafunzi wote na hayimaye wakayoa taarifa kwenye serikali za mitaa ,  Polisi na mtuhumiwa ambaye ilielezwa kuwa ni amekuwa akichunga mifugo katika maeneo hayo  akafikishwa mahakamaini lakini akaachiwa  sababu ya kukosekana kwa ushahidi.

"Mtoto wetu ana umri wa miaka 16 alikuwa amalize darasa la saba mwaka huu wa 2024 nilikuja kujua kuwa ana mimba siku ambayo walimleta hapa nyumbani  walipimwa huko shuleni,  kuna vijana huwa wanachunga mifugo katik maeneo haya  aliwataja kuwa ndio waliomtia mimba mmoja akakamatwa   tukaenda huko kituoni,  tumefika mpaka mahakamani naona ndio wakamwachia  nikaendelea kupambana naye lakini wakasema kuwa hakuna uthibiyisho maalum" alieleza mzazi wa mtoto huyo.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesikiyishwa na kusua sua kwa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya  ya Madanga kwa takribani miaka saba licha ya  vifaa mbalimbali vilivyotolewa  kwaajili ya utekelezaji ikiwemo Mbinge wa jimbo hilo ambaye alitoa mifuko ya saruji pamoja na tofali 500 lakini mradi huo umeahindwa kukilika hadi sasa.

Kutokana na hali hiyo ambayo inawalazimu wananchi wa kata ya Madanga kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya  imemlazimu kuwaomba wadau mbalimbali kujitoa kwa hali na mali kufanikisha ujenzi huo huku yeye mwenyewe akiahidi kuchangia kiasi cha shilingi  Milion 10 .

Akiwa katika kata ya Mkwaja  mwenyekiti huyo amewasisitiza viongozi kusimamia na kukamilisha ujenzi wa ofisi za  chama ngazi ya kata huku akichangia bati 120 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya kata hiyo ambayo ameagiza ikamilike ndani ya mwaka huu wa 2024.

"Hainiingii akilini ndani ya miaka 47 tangu kuzaliwa Chama chetu cha Mapinduzi 'CCM'  chama haikina ofisi za kata haiwezekani tukihitaji vikao vyetu tukafanye kwenye shule za Msingi sio sawa  kisa tu chama ndio kina serikali wajibu wetu tujenge majengo yetu sisi wenyewe  na hatushindwi" alisema

Share To:

Post A Comment: