Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa Ziwa Victoria linakwenda kuwa chanzo Cha maji kwa  Vijiji 33 vya Wilaya ya Bunda na kufanya upatikanaji wa huduma ya Maji kuwa wa uhakika masaa 24 .

Mhandisi Mahundi amesema mtaalam Mshauri amekamilisha usanifu wake na pia serikali  katika kuendelea kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji ina mpango wa kutoa maji kutoka Tanki la Maji Butiama lenye ukubwa wa lita milioni 2.5 katika Mradi wa Majisafi Mugango-Kiabakari kupeleka Nyamuswa kupitia Bisarye.

Mipango hiyo amebainisha akiwa katika Ziara Yake ya kikazi wilaya ya Bunda ya kutembelea mradi wa maji  unaotekelezwa kwa kutumia chanzo Cha ziwa  Victoria kwenye kijiji cha Tiring'ati.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini Mheshimiwa Boniface Getere ameishukru  Serikali kwa uamuzi wa kutumia chanzo cha maji cha uhakika cha ziwa Victoria ili kuboresha huduma ya maji kwenye Wilaya ya Bunda.






Share To:

Post A Comment: