Na  John Walter-Babati   

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema zoezi la  kuhakiki waathiriwa wa maafa ya maporomoko ya udongo,mawe na magogo Hanang' linaendelea ili kuwathibiti wasiokuwa waaminifu wanaotaka kujinufaisha kupitia misaada inayotolewa na serikali kupitia wadau mbalimbali.

Mkuu huyo wa mkoa ameelekeza zoezi hilo lifanyike kwa uwazi kuwatambua walioathiriwa na maafa hayo yaliyotokea Desemba 3 mwaka huu.

Sendiga amesema kuwa ofisi za  kata zitakuwa vituo vya kutolea misaada na kuwaelekeza  waathiriwa wa maafa ambao hawajaorodheshwa  kama waathirika wanaohitaji kuendelea kupatiwa misaada, kufika katika ofisi hizo  kujiandikisha.

Katika hatua nyingine matumaini ya maisha ya awali  kwa wananchi wa wilaya ya  Hanang'  yamerejea  huduma mbalimbali kama maji zimerejea ambapo mkuu wa mkoa anasema serikali inaendelea kurejesha huduma katika maeneo ambayo bado huduma hizi hazipo.

Kwa upande wa miundombinu, Sendega amethibitisha ujenzi wa soko   jipya  kwani  eneo la mwanzo  katika soko la  zamani limebainika kuwa katika mkondo wa maji.

"Tunajenga soko lingine kwa sababu lile soko lililopo pale pameonekana ndio mkondo mkubwa wa maji unapita, maji yameshatengeneza njia  pale yawezekana yakarudi tena  kesho  au keshokutwa, kwa hiyo tumeanza sasa hivi miundombinu ya utengenezaji wa  soko lingine  ambalo tuna imani ndani ya muda mfupi litakuwa tayari na wananchi watarudi kuendelea  kufanya shughuli zao" amema mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga.

Share To:

Post A Comment: