1000463928

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameipongeza
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupeleka msaada wa dawa, vifaa tiba pamoja Msaikolojia Tiba kwa wananchi wa Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang, Mkoani 
Manyara ili kusaidia jitihada za utoaji huduma.

Eneo hilo, lilikumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Hanang na kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo, majeruhi, upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu.

1000463926

Dkt. Yonazi amesema MNH imepeleka mchango ambao una aina mbalimbali (varieties) na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

Akikabidhi dawa na vifaa tiba, Msaikolojia Tiba kutoka MNH Bi. Egla Fugusa amesema msaada huo una thamani ya TZS. 38 Mil.

IMG-20231210-WA0022
Share To:

Post A Comment: