Na John Walter-Babati

Serikali imetoa wito kamati za maendeleo ngazi za kata Pamoja na wadau wa mipango ya maendeleo kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022 katika kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao. 

Wito huo umetolewa na  Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa watendaji na viongozi wa Serikali za mitaa Wilaya ya Babati mkoani Manyara. 

Twange amesisitiza viongozi hao kuacha mazoea ya kutumia makisio na ushawishi wa mtu badala yake wazingatie uwiano na matokeo ya sensa katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.

Amekumbusha sensa ya mwaka 2022  imekusanyanya taarifa Muhimu katika maeneo matatu ambayo ni takwimu za Watu ,Majengo na Anuani za makazi ambayo yote yamesaidia katika usalama wa nchi kwenye masuala ya uhalifu.

Twange amesema Sensa iliyofanywa imesaidia katika mafuriko yaliyotokea HANANG kutokana na baadhi ya waathirika kuingiza vitu ambavyo havikuwemo na kubaini hayo imetokana na sensa ya mwaka 2022.

Amesema matokeo ya sensa ya mwaka 2022 yametoa takwimu ambazo zinarahisisha upangaji wa rasilimali kwenda katika maeneo husika bila upendeleo. 

Naye Mratibu wa Sensa Mkoa Manyara Gidion Mokiwa amesema Ofisi ya taifa ya Takwimu NBS inaendelea kuelimisha makundi mbalimbali kuhusu namna ya kutumia matokeo ya sensa hiyo Ili yatumike katika mipango mbalimbali ya maendeleo. 

Kwa upande wake Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo ameishukuru NBS kwa kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wa Serikali za mitaa ili wayatumie  katika kupanga mipango ya kuhudumia wananchi. 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Manyara Perter Toima, ameiomba ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa mafunzo hayo kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara Kama ilivyofanya katika wilaya ya Babati.

Share To:

Post A Comment: