Na,Jusline Marco:Arusha

Wito umetolewa kwa walimu katika shule ya sekondari ya Ailanga Seminari inayomilikiwa na Kanisa la KKKT Dayosisi ya Meru,Mkoani Arusha kutumia dakika chache zilizobaki kuelekea katika ufanyaji wa mitihani ya taifa ya kidato cha nne,kuendekea kuwa kumbusha na kuwafundisha wanafunzi masomo yao ili waweze kufanya vizuri kwenye mituhani yao.

Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Meru,Mch.Ndelekwa Pallangyo ameyasema hayo wakati akizungumza katika sherehe ya kumbukumbu ya miaka 20 ya shule ya Seminati ya Ailanga na Maafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule hiyo iliyopo Wilayani Arumeru MkoaniArusha.

Mch .Ndekekwa pamoja na kuwaomba walimu kuwafundisha wanafunzi katika siku zilizobaki amewataka wanafunzi hao pia kuongeza bidii kwenye masomo yao na kuwataka pia kujiepusha na makundi yasiyofaa bali wawe vielelezo vizuri katika jamii,familia zao na taifa kwa ujumla huku akiwasihi wazazi na walezi kuendeleza matendo mema waliyonayo watoto wao ambayo wamefundishwa shuleni hapo.

Aidha Mch.Ndelekwa amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa shule ya Ailanga Seminari ni ili kiangaza maisha ya watu jamii na katika Taifa la Tanzania ili shule hiyo iwe mfano wa kuigwa kwani tangu shule hiyo kuanzishwa miaka 20 iliyopia imekuwa nuru kwelikweli.

Ameongeza kuwa mafanikio ya shule hiyo yametokana na baadhi ya watu waliojitoa kwa mali, mawazo na fikra zao ambapo ameushukitu uongozi wa Dayosisi ya Meru chini ya Askofu Elias Kitoi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza Dayosisi na vituo vyote na kuwapongeza viongozi wengine waliopita katika shule hiyo.

"Nieendelea kwa kuwashukuru wazazi kwa kuendelea kuiamini shule hiyo na kuwaleta watoto wenu kusoma na ninaamini wale wote wakao maliza masomo katika shule hii wataendele kuwa kichwa wala hawatakuw mkia kamwe na watakuwa baraka mjini,mashambani,kanisani na hata serikalini."Amesisitiza Mch.Ndelekwa

Mch.Ndelekwa amesema kuwa kufuatia matokeo maziri yanayotoka katika shule hiyo kupitia mitihani mbalimbali,kama Dayosisi imeweka mikakati ni kuondoa daraja 0, daraja la  IV na daraja la III ili kuweza kuyafikia malengo makubwa zaidi waliyojiwekea 

Kwa upande wake Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Meru Paulo Akyo katika maafali hayo ameeleza kuwa lengo la kuanzisha shule hiyo katika eneobla Ngongongare Wilayani Arumeru ni ili kuwafanya wanafunzibkuwa watu wenye faida katika kanisa na jamii nzima.

"Watu ambao watakuwa mianga na nuru ulimwenguni kote, hayo ndiyo malengo yetu kwa seminari hii."alisema Askofu Akyo

Awali akisoma hotuba katika maafali hayo Mkuu wa Shule hiyo Mch.Emmanuel Majora amesema shule hiyo ilianza ikiwa na wanafunzi 45,wavulana wakiwa 29 na wasichana 16 ikiongozwa na viongozi mbalimbali kama walivyopangwa na halmashauri kuu ya Dayosisi na kumshukuru Mungu kwa vipaji vyao katika uongozi.

Mch.Majora ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo hadi sasa miundombinu ya shule hiyo imekuwa ikijengwa kwa njia ya michango ya washarika ,wahisani na wazazi ambapo amewashukuru wote waliojitoa katika kuhakikisha shule hiyo inakuwa na miundombinu bora na rafiki kwa wanafunzi.

Pamoja na mafanikio waliyoyapata upande wa miundombinu ya majengo,maji,barabara na umeme pia shule hiyo imefanikiwa kuwa na Darubini kwa ajili ya kuangalia sayari nyingine hivyo na kufanya kuingia katika idadi ya watu wenye kumiliki Darubini Afrika na hiyo itawasaidia wanafunzi kujifunza baadhi ya masomo yao katika matendo zaidi.

Akieleza takwimu za ufaulu kitaaluma tangu kuanza kwa shule hiyo kuwa jumla ya wanafunzi 1292 ambapo katika miaka 20 ya shule hiyo imeweza kutoa wanafunzi katika ufaulu wa daraja la kwanza 205,daraja la poli 510,daraja la tatu 436 na daraja la nne 141 na kusema kuwa seminari ya Ailanga katika maafali ya kidato cha sita imehitimisha wanafunzi wapatao 323.

"Kuhusu ufaulu huu mpaka leo seminari ina vyeti vya ubora vya serikali 4 na vyeti 5 vya KKKT, vikombe 4 huku baraza la mtihani wakitoa kikombe 1,halmashauri ya Meru 1 na KKKT Dayosisi ya Meru vikombe 2,tunamshukuru Mungu kuwa bado msimamo wa Dayosisi ni kuiendesha seminari hii kwa msingi wa neno la Mungu na kwa maadili ya kanisa."Alieleza Mkuu wa shule hiyo Mch.Emmanuel

Wakisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa Kidato cha nne,mwanafunzi Joshua Mchomvu pamoja na Trina Sia wamesema kuwa walianza kidato cha kwanza walikwa wanafunzi 49,wasichana 30 huku wavulana wakiwa 19 ambapo katika kusheherekea maafali hayo wapo wanafunzi 55 ,wasichana 32 na wavulana 23.

Sambamba na mafanikio waliyoyapata shuleni hapo ikiwemo uwepo wa miradi mbalimbali kwaajili ya kukidhi mahitaji ya wanafunzi na shule kwa ujumla,seminari ya Ailanga inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mabweni,ukosefu wa nyumba ya kudumu ya kufanyia ibada,ukosefu wa jiko na bwalo la kisasa la kilia chakula ,upungugufu wa vitabu na maktaba ya kusomea hali inayosababisha wanafunzi kukosa sehemu ya kujisomea katika maktaba.



Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: