Viongozi wa Dini katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati Mtaa wa Singe wamehimizwa kuwarejesha vijana Makanisani kwani vijana wengi wamekuwa hawahudhurii ibada na wengi wao wamekuwa na maadili yasiyompendeza Mungu.

Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa kanisa hilo Diwani wa kata ya Nangara Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe.Samweli John amesema Kundi kubwa la Vijana wamekuwa hawahudhurii mafundisho ya neno la Mungu jambo linachangia Kwa kiasi kikubwa Ukosefu wa Maadili katika Jamii hivyo Nakuwaomba Viongozi wa Dini kuongeza bidii katika kuwafikia.

Aidha kuhusu Ujenzi wa Kanisa hilo Mhe. Samweli amesema nilazima nyumba ya Mungu iwavutie wengi kuliko kumbi za starehe nakuwataka wamini wa Kanisa hilo kuendelea kuwa na Moyo wa utoaji Ili kumalizia Ujenzi wa Kanisa hilo huku Diwani huyo akichangia Mifuko 20 ya Saruji pamoja na wadau wengine wakifikisha jumla ya Mifuko 130 na fedha taslimu kiasi Cha mil 33.66.

Katika hatua nyingine Mhe. Samweli John ametoa wito Kwa waumini wa Kanisa hilo Kushiriki zoezi la Upandaji wa miti Katika maeneo ya Kanisa huku akiahidi kuchangia Miche miti 100 pamoja na wadau wengine na kufikisha zaidi ya Miche ya miti 600 huku lengo ikiwa ni kukabiliana mabadiliko ya tabia ya nchi.

Naye Mwijilisti Kimambo wa Kanisa hilo amesema Ujezi wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Singe litagharimu zaidi ya mil.500 Mpaka kukamilika kwake na Kutoa wito Kwa waumini kuendelea Kushiriki kuchangia Kwa hali na Mali Ili kukamilisha Ujenzi wa nyumba ya Mungu ambapo zaidi ya waumini 500 wanaweza kuingia Kwa mara Moja wakati wa ibada.

Kwa upande wake Mch.Daniel Gishinde Mchungaji wakanisa la KKKT Mtaa wa mrara amewahimiza waumini wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Singe kuongeza bidii ya uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa hilo Kwa hata Mungu hufurahishwa na kujitoa kwao.







Share To:

Post A Comment: