Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa NBS na Ofisi ya Mtakwimu Zanzibar , Makamisaa wa Sensa pamoja Watendaji wa Benki ya Dunia, jijini Dar es Salaam.


Mchumi Mkuu wa Kanda ya Afrika wa Benki ya Dunia Andrew Dabalen akizungumza katika Kongamano la Kujadili Miaka 15 ya Utafiti uliofanywa wa Kupima kiwango cha Maisha , jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande akizungumza kwenye kongamano la kujadili masuala mbalimbali yaliyojiri wakati wa utekelezaji wa tafiti zilizofadhiliwa chini ya mradi wa Benki ya Dunia uliokuwa unapima kiwango bora cha maisha (Lving standards Measurement study-intergrated survey on Agriculture(LSMS-ISA) lililofanyika jijini Dar es Salaam.


Matukio mbalimbali ya picha wakati wa kongamano la kujadili tafiti ya kupima kiwango cha maisha uliofanywa kwa miaka 15.



Na Chalila Kibuda
UTAFITI unaonyesha kiwango cha umasikini wa upatikanaji wa chakula kimepungua Tanzania.


Kupungua huko kunaifanya nchi kuwa katika kiwango bora cha maisha kutokana na kufatilia kaya , familia kwa miaka 15 katika utafiti huo.

Hayo yamebainisha jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande kwenye kongamano la kujadili masuala mbalimbali yaliyojiri wakati wa utekelezaji wa tafiti zilizofadhiliwa chini ya mradi wa Benki ya Dunia uliokuwa unapima kiwango bora cha maisha (Lving standards Measurement study-intergrated survey on Agriculture(LSMS-ISA) lililifanyika jijini Dar es Salaam.

Utafiti huo unefanya Tanzania kufanya maadhimisho ya miaka 15 ya kufanya utafiti ya hali ya umaskini hapa Tanzania na katika Bara la Afrika na nchi nyingine kushiriki juu utafiti huo.

Amesema programu hiyo ya utafiti iliyoanza 2008 ambayo ilifadhiliwa na benki ya Dunia imeleta msaada mkubwa wa kutambua hali ya upatikanaji wa chakula nchini na matokeo yake yamekuwa chachu kutokana na serikali kuweka sera na mikakati yake kuinua wananchi kiuchumi.

"Kiwango cha umasikini kwa sasa kimepungua hasa umasikini wa upatikanaji wa chakula,chakula kipo kwa wingi cha kutosha ambapo sisi watanzania leo tunazalisha chakula tunapeleka nchi jirani,"amesema Chande

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa amesema miaka 15 ya utafiti huo umeleta mafanikio makubwa ndani ya Bara la Afrika.

Amesema utafiti huo umefanywa kwa kufuatilia kaya moja baada ya nyingine kwa muda wa miaka 15 umewezesha serikali yakupunguza hali ya umasikini hususani vijijini kwa kuweka miradi mbalimbali ikiwemo kilimo kwa kupeleka pembejeo.


Amesema kupitia utafiti huo umeiwezesha serikali ya Tanzania na serikali nyingine za Afrika kupunguza umaskini wa chakula.

"Takwimu hizi zimetumika kwenda kwenye program za kuwawezesha watanzania waonyonge hasa maeneo ya vijijini,"amesema Dk Chuwa.

Amesema wakati utafiti unaanza 2008 katika Bara la Afrika nchi nyingi zilikua zinafanya utafiti kwa kutumia karatasi lakini sasa teknolojia imekuwa na sasa utafiti unafanywa kwa kutumia vishkwambi.

Naye ,Kamisaa wa Sensa Anna Makinda amewataka watafiti kurudisha tafiti hizo kwa wananchi kwa maana wao ndio wahusika wakuu wa kuweza kutumia kwa tafiti zikifanywa na kuweka katika ofisi haiwezi kuinesha hali halisi ya utafiti ulivyofanyika.

Amesema utafiti huu umefanikiwa kwa sababu umeweza kumfikia mtu mmoja mmoja na kuelezea ukweli kuhusu maisha yake jambo ambalo si rahisi.

"Hawa wataalam wa takwimu tunasema sasa wakati umefika utafiti wao uenze kuwatumikia hawa wananchi lakini pia utasaidia utendaji wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake"amesema Makinda.

Kwa Upande wake, Mchumi Mkuu wa Kanda ya Afrika wa Benki ya Dunia Andrew Dabalen amesema serikali ziwekeze zaidi kwenye utafiti na kuwa na mfuko maalum kwaajili ya utafiti ni muhimu.
Share To:

Post A Comment: