Na John Walter-Babati
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amezindua mradi wa maji wa kijiji cha Hoshan kata ya Duru wilayani Babati , wenye thamani ya shilingi Milioni 319,759,419.
Akizungumza na wakazi wa Hoshan mara baada ya kuzindua mradi huo Sendiga amesema mradi huo ni mojawapo ya malengo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwaondolea wananchi adha ya kukosa maji.
Aidha ameagiza wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Mkoa wa Manyara kuongeza idadi ya vituo vya kuchotea maji kijijini hapo ili huduma ya maji iwafikie wengi ikiwa ni maeneo ya taasisi za serikali kama shule, Zahanati na nyumba za ibada.
Kwa mujibu wa meneja RUWASA wilaya ya Babati Mhandisi Felix Mollel, Mradi huo umeanza kutoa huduma na una uwezo wa kuwahudumia wananchi 2,660 kila siku.
Naye Mbunge wa jimbo hilo Daniel Sillo amesema ataendelea kuwasemea wananchi ili maeneo ambayo hayana huduma ya maji wafikishiwe na serikali.
Post A Comment: