Katika kile kinachoelezwa kuwa mapinduzi ya nishati ya umeme, wananchi hasa wa maeneo ya vijijini wamechangamkia fursa kutumia nishati hiyo kujiletea Maendeleo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu anasema nishati hiyo imewezesha wengi kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ziara ya REA na Wabia wa Maendeleo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini, Kingu amesema uwepo wa Umeme wa uhakika umechochea Maendeleo maeneo ya vijijni.

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA) Mhandisi Jones Olutu amesema serikali imeweza kufikisha huduma hiyo kwa wananchi kwa kushirikina na wabia kutoka nchi mbalimbali kwa sababu kiongozi mkuu wa nchi amejenga mahusiano mazuri na mataifa duniani.

Amesema REA na wadau wengine watakuwepo Manyara kwa siku tatu kwa ajili ya mkutano mkuu wa Mwaka na kuangalia namna mradi ulivyotekelezwa mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ametoa pongezi kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri ya kuendelea kusambaza umeme pamoja na aina nyingine za nishati.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha kuwa inapeleka Umeme kwenye maeneo yote ya uzalishaji mali, utoaji huduma za Afya, zahanati, pump za maji na viwanda vidogo vidogo.
Share To:

Post A Comment: