Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ngorongoro ambapo ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kukagua thamani ya halisi ya fedha.

Rc Mongela ameyasema hayo baada ya kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la utawala katika Halmashauri hiyo ambalo limekamilika kwa asilimia 88 huku ujenzi wake ukiwa umegharimu kiasi cha shiliongi bilioni 2.6 jengo hilo limejumuisha nyumba ya walinzi, chumba cha kusambazia umeme, maegesho ya magari, barabara pamoja na taa za ulinzi.

Akiwa  ziara hiyo mkuu wa mkoa amewasisitiza watumishi wa Halmashuri ya kuwa  nidhamu,usimamizi mzuri wa miradi sanjari na ufuatiliaji wa karibu wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndio unaopelekea miradi ya kimaendeleo kukamilika kwa wakati ikiwemo ushirikishwaji wa wataalamu ili kusogeza huduma za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo Rc Mongela amepongeza Mkurugenzi wa halmshauri hiyo Nassoro Shemzigwa na sambamba na Mkuu wa wilaya hiyo, Raymond Mangwalla kwa usimamizi mzuri wa  ujenzi wa jengo hilo ambalo  hapo awali ujenzi wake ulikuwa ni wakusuasua.

Awali katika ziara hiyo Rc Mongela aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwachulia hatua za kisheria waliokuwa wasimamizi wa mradi wa shule ya Sekondari Sero katika Kata ya Ololosokwan kwa kusababisha mifuko 886 ya saruji kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha akiwemo Mkuu wa shule mama ya sekondari Soitsambu, Mwl. Alex Masawe na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Sero Ally Mrisho.

Mhandisi Masasila Chiguru ni msimamizi wa mradi huo wa jengo la utawala ambapo amesema jengo hilo limetekelezwa kupitia 'Force Account' chini ya Mkandarasi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) huku mradi huo ukitekelezwa kwa awamu ya tatu na tayari umefikia asilimia 88 ya utekelezaji wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri Nassoro Shemzigwa amesema wamepokea maelekezo yote ya Mkuu wa mkoa pamoja na changamoto zilizopo watahakikisha wanayafanyia kazi kwa wakati ili kuweza kukamilisha miradi yote kwa mwaka huu wa fedha sambamba na thamani ya fedha inaonekana.




Share To:

Post A Comment: