Na Mwandishi Wetu; Songea

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amezindua mwongozo utakai wawezesha wanachama kujua haki pamoja na mafao yao.


Mwongozo huo umezinduliwa leo tarehe 27 Novemba, 2023 mkoani Ruvuma katika viwanja vya Ofisi ya Hazina ndogo iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,



Amesema kwa mwaka 2019 hadi 2023 serikali imelipa wastaafu jumla ya sh. Trilioni 2.17 ambapo makusudio ni kuhakikisha wanapata mafao yao kwa wakati.


"kisheria wastaafu wanatakiwa kulipwa fedha ya kustaafu kutokana mshahara wake wa mwisho ambapo mwajiri anatakiwa kupeleka mchango mwezi mmoja baada ya mshahara wake"


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Wilman Ndile alisema kuzinduliwa kwa mpango huo kutasaidia kupunguza kero za wastaafu zinazofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii .
  

Naye Mkurugenzi wa Undeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mbaruku Magawa amesema kuwa mwongozo huo utawasaidia wastaafu kuhakiki nyaraka zao.


Kwa niaba ya wastaafu Nd. Amen Ally atoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali Wastaafu na kutatua kero zao.


Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: