Na John Walter-Hanang'

Jeshi la Polisi Wilaya ya Hanang' Manyara limefanya ukaguzi wa vyeti vya udereva kwa madereva wa daladala na mabasi ya abiria ili kuwabaini wasiokuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo.

Operesheni hiyo ya kukagua vyeti kwa madereva wa daladala na magari makubwa ya abiria ili kuhamasisha madereva kwenda shule na kuzuia ajali za barabarani.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Novemba 24, 2023 katika stendi kuu ya mabasi Kateshi Mkuu wa Kikosi Cha Usalama barabarani wilayani humo Mkaguzi wa Polisi (INSP) Volca Willa amesema uhakiki huu ni katika kuhakikisha madereva wote wa abiria wanapata mafunzo katika vyuo vya udereva vinavyotambulika na serikali.

Ameeleza dereva aliyapata mafunzo na kufaulu huwa mtumiaji nzuri wa barabara kwani ataendesha kwa kuzingatia Sheria na kanuni za usalama barabarani

Jumla ya Madereva 89 na vyeti 120 vimehakikiwa na zoezi litaendelea mpaka mwishoni mwa mwaka 2023.

Share To:

Post A Comment: