Niungane na wananchi wenzangu wa wilaya ya Same na Tanzania kwa ujumla kuwatakia watoto wetu Mtihani mwema, imani yetu ni kubwa tunategemea matokeo mazuri hasa kwa wilaya yetu kwakua Elimu ni miongoni mwa vipaumbele kwa serikali na sisi wilaya ya same tulikwisha jiandaa mapema. 


Jumla ya wanafunzi 4368 wameandikishwa kufanya Mtihani wa taifa wa kidato cha nne kwa mwaka 2023 katika wilaya yetu ya Same pekee, mitihani iliyokwisha anza Novemba 13 mwaka huu ambapo kati ya wanafunzi hao wavulana ni 1766 na wasichana ni 2602.


Nimepata wasaa wa kutembelea baadhi ya shule ambako wanafunzi wanaendelea na Mitihani hiyo ya mwisho kuhitimu kidato cha nne ambapo mpaka sasa hakuna changamoto yoyote Mitihani inaendelea kwa amani na utulivu kama ilivyo pangwa kwakua tumeimarishwa ulinzi na usalama maeneo yote kuwawezesha wanafunzi hao kufanya mitikani yao kwa utulivu.

 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: