Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb), ameshuhudia hafla ya utiaji wa saini wa utekelezaji wa mradi wa maji eneo la Kusini Mwa mkoa wa Dar es Salaam unaotekelezwa na DAWASA kwa gharama ya shilingi bilioni 40
Katika hafla hiyo, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Awesso ndiye aliyekuwa mgeni rasmi pia viongozi mbalimbali wakiwemo waheshimiwa wabunge wa maeneo husika, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam waliweza kushiriki hafla hiyo
Mradi huu utahudumia wananchi takribani 450,000 wanaoishi katika majimbo ya uchaguzi ya kibamba, segerea, ukonga na temeke.
Post A Comment: