Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Jumanne Mlagaza akiongoza, kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha 2023/2024 kilichoketi leo Novemba 3, 2023.

..................................................


Na Dotto Mwaibale, Manyoni

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, limesikitishwa na Wakala wa Usambazaji Maji na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani humo kutokamilisha mradi mkubwa maji ujulikanao kama Kintiku Lusilile unaolenga kuhudumia vijiji 11 unaogharimu kiasi cha Sh.Bilioni 12. 

Madiwani hao wametoa masikitiko hayo katika kikao cha kawaida cha baraza hilo cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha 2023/2024 wakati wakijadili taarifa ya RUWASA. 

 Katika kikao hicho cha madiwani kilicho hudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Dk. Pius Chaya wamekashangazwa mradi huo kutokamilika kama mkataba ulivyosainiwa ambapo ilitakiwa kazi ya ujenzi wa mradi huo iwe imekamilika ifikapo mwezi huu wa Novemba ambapo umesogezwa mbele hadi Januari 2024. 

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya  hiyo  Jumanne Mlagaza akiongoza kikao hicho,amewataka madiwani  kusimamia vyema miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miradi hiyo inakidhi thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa miradi hiyo.

 “ Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi hii fuatilieni kwa ukaribu kwani kumekuwa na udanganyifu kwenye baadhi ya maeneo ambapo mara kadhaa miradi hukamamilika na kukabidhiwa ikiwa haijakidhi vigezo pamoja na thamani halisi,” alisema Mlagaza.

Aidha,  baraza hilo la madiwani limemfuta kazi Muuguzi Msaidizi, Atieno Otieno kwa sababu za utoro kazini. 

Akitoa taarifa hiyo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jumanne Mlagaza alisema baraza hilo limefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mfanyakazi huyo aliyekuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya hiyo ameenda kinyume na sheria. 

"Kwa mujibu wa sheria mtu anapokosekana siku tano katika kituo chake cha kazi bila ya kuwepo kwa taarifa yoyote  anakuwa amekiuka mashariti ,hivyo kuanzia leo kikao hiki cha madiwani kimeridhia kumfukuza kazi na kuanzia sasa  Atieno sio mfanyakazi wa halmashauri hii,” alisema Mlagaza.

Kikao kikiendelea.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Dk. Pius Chaya, akichangia jambo kwenye kikao hicho.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail.
Uchangiaji ukiendelea kwenye kikao hicho.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: