Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila akiongea na wanamichezo wakati wa uzinduzi wa Uwanja Wetu Project uliopo Kijiji cha Kipara Mtua


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

HALMASHAURI ya wilaya ya Nachingwea imepanga kujenga uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa kutokana na mapato ya ndani ya msimu huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja Wetu Project uliopo katika Kijiji cha Kipara Mtua, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila alisema kuwa watajenga uwanja wa kisasa Kwa lengo la kukuza vipaji vya mpira wa miguu na michezo mingine.

Mpyagila alisema kuwa haiwezekani watu wachache waweze kujenga uwanja mzuri kijijini halafu Halmashauri ikashindwa kujenga uwanja wa kisasa wakati mapato ya ndani tu wakati ardhi ya Nachingwea imebarikiwa kuwa na madini ya Kila aina ambayo yanachagia fedha nyingi.

Alisema kuwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea itachangia mifuko 100 ya Saruji Kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja huo ambao Kwa sasa ndio kivutio cha michezo wilaya ya Nachingwea.

Mpyagila alimazia kwa kuwapongeza viongozi wa Uwanja Wetu Project Kwa kuwa na wazo chanya lenye lengo la kuinua vipaji vya michezo Nachingwea kwa ujenzi wa kisasa wa Uwanja Wetu Project.


Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuja la wazo la ujenzi wa Uwanja wa kisasa kwa ajili ya michezo na kukuza uchumi wa wananchi wa Halmashauri hiyo 

Walisema kuwa ukijengwa uwanja huo utakuwa umesaidia kukuza uchumi na vipaji vya michezo na kurudisha hamasa ya michezo kwa wananchi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: