Julieth Ngarabali ,Pwani. 

Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Pwani imeelekeza watumishi na wataalamu wa Serikali Mkoani humo kuhakikisha  wanakamilisha miradi yote ambayo bado haijakamilika ifakapo Desemba mwishoni mwaka huu kwani fedha zake zilishatolewa na Serikali kuu.

Miradi hiyo ni pamoja na ya afya, Elimu  na miundombinu,maji, umeme na barabara kwani Serikali ilishatoa fedha  za ujenzi wake, lakini  katika ziara  iliofanywa na kamati ya siasa Mkoani humo  imebainika bado haijakamilika kwa asilimia mia ni mingi imefikia asilimia 98 tu ya utekelezaji wake.

Maelekezo hayo yametolewa kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho  kwa kipindi cha Machi 21 /2021 hadi Juni 2023 na kwamba wasilisho hilo lilipokelewa na wajumbe hao kwenye ukumbi wa mikutano ya shule ya Mwalimu Julius Nyerere Kwamfipa Kibaha.

"Tumefanya ziara kamati ya siasa katika Halmashauri zote kasoro Mafia na tumeona kuwa miradi hiyo imefikia asilimia 98 ya utekelezaji na sehemu zilizobakia ni ndogo sana ambazo ni za kumalizia tu hivyo tunaelekeza Desemba mwishoni iwe imekamilika kwa asilimia mia "amesema Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Benard Ghaty 

Amesema katika  utekelezaji huo wameona mwenendo wake unaenda kwa ufanisi na kinachotakiwa ni kuendeleza ufanisi huo ili kwenda sawasawa na uhalisia wa pesa zilizotolewa na Serikali.

Akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kamisaa Abubakari Kunenge ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo amesema Mkoa huo ulipokea sh . 1.19 Trilion  katika kipindi cha 2021/2022 na Januari/Juni 2023 kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo  kamati ya siasa imepita kukagua na kuona maendeleo ya ujenzi wake 

" Katika kikao hiki sisi tumewasilisha taarifa ya miradi yote ambayo hata mingine kamati ya siasa haikuweza kupita na tumeamua kutumia utaratibu wa teknorojia ambapo hata maeneo ambako wajumbe hawakufika wameweza kuona kwa sababu tulichofanya sisi tumeeleza ibara inasema nini kwa sababu ukiangalia Ilani imetoa maelekezo yaliyo mahususi na maelekezo yaliyo ya jumla hivyo tumesema kwa kila Idara Serikali imefanya nini"amesema.

Na kuongeza "tunamshukuru Rais kwakuwa mlezi mwema wa kutuongoza na kutufundisha namna ya kuhudumia wananchi na sisi kama wasaidizi wake kwa kushirikiana na watendaji wengine wakiwemo wabunge kwa sababu shughuli zilizofanyika bila kupitishwa kwa bajeti zisingetekelezeka"amesema Kunenge 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwishehe Mlao amesema  ili kwenda na wakati kuna ulazima wana CCM  kubadilika na kwenda na wakati kwa kuzingatia muda wa utekelezaji wa majukumu yao na hata kuhudhuria vikao 

"Niwakumbushe wajumbe tusiendelee na zama zilizopita ni vema tukabadilika hususan katika kujali muda wa utekelezaji wa majukumu yetu na si kubaki na zama za karne zilizopita, kama ni saa fulan Kuna jambo hili tuzingatie muda " amesema

Awali baada ya  kuwasilishwa kwa taarifa hiyo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kamati ya siasa ilitoa mapendekezo manne kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ikiwemo kumpongeza Rais Samia  Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akielekeza fedha kwenye miradi mikubwa ikiwemo ya kimkakati mkoani Pwani

Mapendekezo mengine ni kumpongeza Mkuu wa Mkoa Kunenge kwa kusimamia utekelezaji wa miradi iliyokaguliwa, Viongozi wa CCM ngazi zote kwa  kushirikiana na wataalamu kusimamia miradi hiyo na kutaka ipokee wasilisho hilo na itoe nguvu kwa watendaji wa Serikali kukamilisha pale ambapo mingine hawajakamilisha.

Ikumbukwe kwamba Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa ya kimkakati ambapo baadhi ya miradi inayotekelezwa ni pamoja na wa  umeme kutoka bwawa la Mwalimu Nyerere na barabara ya njia ya nne ya Kimara/Kibaha

Share To:

Post A Comment: