Ashrack Miraji Same kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amezindua kampeni maalum ya upandaji miti kwenye Wilaya ya Same mwendelezo wa mkakati wa utekelezaji wa mpango wa Serikali kutunza mazingira hasa maeneo ya vyanzo vya Maji na kuvutia Utalii.

Zoezi hilo ni utangulizi wa Tamasha la Utalii Same maarufu SAME UTALII FESTIVAL lililopangwa kufanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Disemba Mwaka huu 2023.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Mkuu wa wilaya amesema zoezi hilo linaanzia kwenye Taasisi za Serikali zikiwemo Hospitali,vituo vya Afya na Shule pia kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vyanzo vya maji na watu binafsi.


"Tunapozungumzia Utalii,tunazungimzia wanyama ambao wanahitaji mazingira mazuri ili waweze kustawi na kuendelea kuwepo,hivyo tunaotesha miti ili kustawisha uwepo wa wanyama ambao ndio wanaovutia Utalii".Amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha amewataka wananchi wa Wilaya ya Same kuunga mkono juhudi za Serikali za kutunza mazingira kwa kila kaya kuotesha miti mitano hasa kila unapofika msimu wa mvua.

Mkuu wa Wilaya pia aliishukuru Kampuni ya Tanzania Footmark Safari kwa kuchangia miti laki moja ili kufanikisha zoezi hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amesema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha kuwa Wilaya inafikia lengo la kuotesha miti mil 1.5 kila mwaka.

"Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa miti yote inayooteshwa inastawi na tunazo Sheria ndogo za kuhakikisha wale wote wanaolisha mifugo katika maeneo yaliyooteshwa miti wanachukuliwa hatua maana mifugo ndio inayoharibu miti yetu"amesema Bi.Tutuba.

Mkurugenzi huyo ametoa shukrani kwa Taasisi na mashirika yanayowezesha miche ya miti Wilayani humo wakiwemo Wakala wa Misitu nchini (TFS),shirika la FLORESTA na Same NG'Os 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: