Na John Walter-Babati

Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao wanaoishi kwenye vyumba vya kupanga maarufu kama Gheto kwa kuwa ni chanzo cha vishawishi vinavyopelekea kukatisha ndoto zao za kuendelea na elimu.

Wito huo umetolewa na afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Manyara Mugisha Galibona wakati akizungumza kwa niaba ya Katibu tawala Mkoani hapa katika kilele cha juma la Elimu iliyofanyika katika shule ya Sekondari Ufana.

Aidha amepongeza uongozi wa Shule hiyo Kwa kuanzisha jukwaa hilo la kila mwaka huku akiwataka Wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto hasa wanaoishi nje na Nyumbani na kuwaagiza Watendaji na Maafisa elimu ngazi ya kata kujua utaratibu unaotumika katika upangishaji wa nyumba Kwa wanafunzi.

"Natoa wito Kwa Viongozi wakiwemo Maafisa Elimu kata kuweka utaratibu wa kufahamu nyumba zinazopangishwa na wanafunzi kama zinaendana na yanayofanyika huko maana isije ikawa mzazi anachangia na huku moto anachukuwa hela Kwa mtu mwingine matokeo yake mtoto anaharibika" alisema Mugisha

Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Secondari Ufana Mwalimu Haikasia Minja amesema  Juma la elimu limeanzishwa Kwa lengo la kuongeza taaluma katika Shule hiyo kwani mpaka sasa wamefanikiwa kupunguza Utoro na Wazazi kujua mwenendo wa tabia za watoto wao pamoja na kuongeza ushirikiano baina ya Walimu na Wazazi katika Kushiriki kuchangia maendeleo ya Shule hiyo.

Minja amesema wanafunzi hupata fursa ya kufanya maonyesho ya kitaluma pamoja na Masomo ya stadi za Maisha na ujasiriamali kwani wanafunzi hushiriki kutengeneza sabuni pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana ukatili wa kijinsia.

Amesema Kupitia Juma la elimu Shule imekabidhiwa Baiskeli 50 kutoka Kwa wadau wa maendeleo na kugawiwa Kwa wanafunzi waishio mbali huku pia Shule ikipatiwa Computer 20 pamoja na Bati 120 kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za watoto wa kike wa kidato cha Tano na sita.

Kwa upande wao Wazazi wenye wanafunzi katika Shule hiyo wamepongeza uongozi wa Shule Kwa juhudi zao za kuinua Taaluma Kwa watoto wao kwani Kupitia Juma la elimu Wazazi wametambua wajibu wao wa ushiriki katika kuboresha miundombinu ya Shule ya Secondari Ufana.


Share To:

Post A Comment: