Akizungumza wakati wa kuhitimisha Juma la elimu mkuu wa Shule ya Secondary Ufana Mwl. Haikasia Minja amesema jumla ya wanafunzi 7 waliofanyiwa ukatili wa kingono wamerejeshwa Shuleni akiwemwa mwanafunzi aliyefanyiwa ukatili huo na Baba yake Mzazi amba Kupitia Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Babati mwanafunzi huyo alihamishwa Shule na kutafutiwa ufadhili Ili aweze kutimiza ndo zake.

Ameyasema hayo wakati wa kilele cha kuhitimisha Juma la elimu inayoadhimishwa Kila mwaka katika Shule hiyo Kwa lengo la kuwakutanisha Wazazi na walezi ili kuinua hali ya Taaluma na kutokomeza daraja (0) na kudhibiti hali ya Utoro na Kutoa elimu Kwa Wazazi na walezi juu ya namna ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

Aidha Mwl. Minja ameongeza kuwa hali ya ufaulu imeongezeka kutokana na wao kufundisha vipindi vya ziada pamoja na Kutoa zawadi Kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika Masomo yao hasa katika kipindi cha kuadhimisha Juma la elimu.

Sanjari na hayo Mwl. Minja ameiomba Serikali kuharakisha uanzishwaji wa Kidato cha Tano na Sita Kwani Kwahivi sasa Shule inamadarasa ya kutosha kutokana na kujengwa Kwa Shule Mpya katika kata ya Secheda ambayo inatarajiwa kuanza mwaka 20234.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Secheda Mhe.Ibrahim Tatock ameahidi kushirikiana na kamati ya maendeleo ya kata ili kutatua changamoto ya uhaba wa maji kwakuwezesha tenki 2 ya kuhifadhia maji ifikapo mwezi wa 12 mwaka huu.

Naye Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Manyara Mwl. Kamugisha Galibona Kwaniaba ya Katibu tawala Mkoani hapa ameongeza kuwa  uanzishwaji wa wiki ya elimu katika Shule hiyo na Kutoa wito Kwa Wazazi pamoja na walezi kushiriki kikamilifu katika kuboresha mazingira ya  Shule Kwa lengo la kuongeza ufaulu na kuondoa Alama (0)

Hata hivyo Shule ya Secondary Ufana Kupitia maadhimisho ya Juma la Elimu imefanikiwa kuwaunganisha Wazazi na uongozi wa Shule hiyo jambo liliongeza ubora wa Taaluma na kuongeza ufaulu mwaka Hadi mwaka.

Share To:

Post A Comment: