Maji yana umuhimu kwa binadamu kwa sababu asilimia 50-65 za mwili wa mwanadamu ni maji hata miili ya mimea na Wanyama kwa kiasi ni maji ambapo pia robo tatu ya dunia maji ambapo yamechukua asilimia (71.11) hivyo maji ni kitu cha msingi sana kwa dunia na wanadamu.
Kwa muda mrefu, serikali imeendelea kutoa huduma ya maji safi kwa kupeleka miradi ya maji vijijini ili kuwapunguzia wananchi adha ya kukosa maji katika maeneo yao ila miradi mingi imeshindwa kukamilika kwa wakati na miradi mingine kutofanya kazi kabisa kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo kutosimamiwa vizuri na kukosa matengenezo muhimu.
Upungufu huu umesababisha kuhitajika kwa mpango thabiti na endelevu wa uratibu na usimamizi wa utoaji wa huduma hii katika ngazi za kitaifa, mkoa na wilaya. Serikali inaendelea kutekeleza sera na mkakati unaowezesha majukumu mbalimbali yakutekelezwa katika ngazi husika.
Pamoja na sehemu mbalimbali kuboreshwa mijini na vijiji kwaajili ya maji bado hali ni tete vijini kwani Asilimia 46% ya watu wa vijiji ndio hunafaika na mijini ni 74% hii hudhirisha changamoto ya maji.
Hata hivyo pamoja na maji kuonekano ni muhimu kwa binadamu bado ni changamo katika maeneo ya vijijini shughuli zao nyingi hutegemea maji hasa katika kilimo,ufugaji ambapo wafugaji hujengewa mabirika na mabwawa ya kunywesha mifugo kipindi cha kiangazi sambamba na shughuli za binadamu ambazo huchangia mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo husababisha ukosefu wa maji hii ikiwa na maana vijijini hutegemea vyanzo vya asili visivyo salama uchunguzi wa wanachi katika mikoa ya Arusha Mara,Kilimanjaro umebaini hali sio shwari licha ya mikakati mingi ya serikali ya kuhakikisha huduma hiyo inasambaa nchini kote.
Hali ya upatikanaji wa maji katika vijiji vingi katika Mkoa wa Arusha siyo wa kuridhisha ambapo kwa mujibu wa takwimu maeneo ya vijiji vya mkoa huu upatikanaji wa huduma unafikia asilimia chache sana.
Kiwango hicho ni ongezeko la zaidi ya asilimia mbili kulinganisha na wastani wa asilimia 72.3 ya mwaka 2021, hali inayoashiria kuna uwezekano wa kufikia lengo la maji kupatikana kwa asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara ya maji kwa mwaka wa fedha 2022/23, hadi kufikia Aprili, 2022 hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini ilikuwa ni wastani wa asilimia 86.5 ikilinganishwa na asilimia 86 ya mwezi Machi 2021 huku lengo ikiwa ni kufikia asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.
Samweli Mesieki ni mkazi wa Kijiji cha Engutoto wilayani Monduli ambapo anaeleza kuwa kutopatikana kwa huduma ya uhakika ya maji safi na salama siyo tu kunasababishawatu kutumia muda mwingi kusaka maji badala ya uzalishaji, bali pia ni tishio la kiafya kutokana na baadhi ya watu kutumia maji yasiyo safi na salama.
“Maji yanatoka kwa mgawo asubuhi au jioni mara mbili kwa wiki na yakitoka tunaacha kila kitu ili tukinge na kuhifadhi maji ya kutosha kwa siku mbili hadi tatu na bado ankara inakuja kubwa” Alisema
“Hata sasa kuna changamoto ya umeme na unafahamu serikali yetu vyanzo vyake vingi vinazalisha maji kwa kutumia umeme, kwa hiyo bado tupo kwenye changamoto ya umeme na maji.” Aliongezea
Abdala Salim ni mfanyabiashara ambaye mkazi wa Monduli Juu ambapo amesema huduma ya maji eneo lao bado ni changamoto kubwa inayowatesa kwani anategemea maji katika shughuli zake za biashara ya mgahawa ambapo kukosekana kwa maji muda mrefu kunamkosesha wateja kwani muda mwingi anakuwa amefunga biashara kwenda kutafuta maji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilayani Ngorongoro amekiri kuwepo kwa tatizo la upatikanaji wa maji, akitaja ukame kuwa chanzo cha changamoto hiyo katika baadhi ya maeneo nchini kilichosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Rais Samia Suluhu Hassan amenukuliwa mara nyingi akieleza kuwa anatambua matatizo yanayowakabili kina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji, hivyo Serikali itahahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 tatizo la maji nchini linakuwa limekwisha kwa kumtua mama ndoo kichwani.
Kwa upande wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameeleza kuwa Serikali inatekeleza malengo ya kuhakikisha huduma ya maji yanapatikana kwa asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini ifikapo 2025
“Maji hayana mbadala, ni lazima maji yapatikane popote yalipo bila kujali gharama” Aalisema.
Aidha maji hutumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo umwagiliaji wa mashamba na mazao matumizi manyumbani sambamba na kunyweshea mifugo hivyo ni vyema serikali kuangalia namna bora ya kuwachimbia mabwawa wananchi ambao bado wanatumia muda mwingi kwenda kutafuta maji na kuacha kufanay shughuli za kimaendeleo ambazo huwa ndizo zinazowaingizia kipato.
Serikali kupitia RUWASA Mkoa wa Arusha katika kipindi cha bajeti 2021/2022 ilitenga fedha kwa ajili ya kujenga miradi mipya kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji maji vijijini, ambapo jumla ya miradi 66 yenye thamani Tsh.32,610,648,952.64
Katika bajeti ya 2021/2022 RUWASA Mkoa wa Arusha iliidhinishiwa jumla ya Tsh.10,276,348,023 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini, hadi sasa jumla ya Tsh.4,396,637,286.90
Hata hivyo, jukumu la maji si la serikali peke yake, Katika baadhi ya maeneo watumiaji wengi wa maji wengine bado wana dhana kuwa jukumu la kuwapatia wananchi huduma ya maji ni la Serikali pekee, kama ilivyokuwa hapo awali. Aidha, katika baadhi ya maeneo, kuna mwamko usioridhisha kwa watumiaji maji kuchangia katika gharama za ujenzi na uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji. Ni muhimu wote kutambua nafasi zetu ili kwa pamoja tuweze kufika asilimia 100 ya upatikanaji wa maji safi na salama, huku tukitunza mazingira ili upatikaji huo uwe endelevu.
Post A Comment: