Na , Carlos Claudio - Dodoma

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema atawafutia leseni mabroka wote watakao kiuka taratibu zilizowekwa na serikali pamoja na watakaojihusisha na utoroshaji wa madini.

Mh.Mavunde amesema hayo leo Oktoba 19,2023 Jijini Dodoma katika kikao cha pamoja na Chama cha Mabroka wa Madini Tanzania (CHAMMATA).

Amesema serikali inawatambua mabroka wote kwa mujibu wa sheria ndio maana wanapewa leseni na anatamani kuwaona mabroka wananufaika kwani ni watu muhimu katika mnyororo wa biashara ya madini.


“Iwapo itathibitika mnashirikiana na dealers kutorosha madini hapo mtaacha kuwa marafiki zangu na hivi sasa tukimkamata mtu mmoja nafwatilia mnyororo mzima sitamuachi mtu hata mmoja.”

Na kuongeza kuwa “Madini yakitoroshwa serikali ikipoteza mapato tutashindwa kujenga barabara, tutashindwa kununua madawati, tutashindwa kununua madawa hivyo mtu yeyote anaye ipenda na kuijali nchi yake atalipa uzito jambo hili , msikubali kuwa ngazi ya kuwakosesha madawa , kuwakosesha barabara nzuri, kuwakosesha madawati watanzania hivyo nataka ukikaa peke yako ujitathmini.” amesema Mh. Mavunde.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Mabroka wa Madini Tanzania Jeremia Kituyo amesema CHAMMATA kilianziwa tarehe 13,2022 Jijini Dodoma lakini hadi hivi sasa wana mabadiliko ya kuwa na wanachama mabroka wenye leseni na wasio na leseni 18,638 nchi nzima licha ya kuhamasisha mabroka wote wapate leseni ili kufikia malengo ya wizara ya madini na wafanye biashara kihalali.

“Aidha kitendo cha serikali kuzuia madini ya Tanzanite kuuzwa mikoa mingine tofauti na Mererani imesababisha masoko mengine nchini kudorora hasa soko la kitaifa la Mkoa wa Arusha kwani soko la Arusha ni la kimataifa na ni soko linaloleta madini kutoka nchi za jirani ni soko ambalo lilikuwa limechangamka kupokea madini kutoka mikoa yote nchini lakini hivi sasa soko la Arusha limeharibika alkadhalika soko la Dar es salaam limeharibika pia.”

Na kuongeza kuwa “Ukuta uliojengwa na serikali ule ukuta tuna uthamini , tunaupenda na uendelee kuwepo ni ukuta ulioleta nidhamu kwa wafanyabiashara na kwa wachimbaji, siku za nyuma walikuwa hawana nidhamu kibishiara na mali yetu hivyo ukuta ule ni wa maana sana kwa sisi wafanya biashara na watu wanaingia ndani ya ukuta kuanzia saa12 asubuhi na kutoka saa 3 au saa 4 usiku na mji wa Mererani yani umekuwa kama bahari kwa sababu kila kitu kinafanyikia mule ndani.” alisema Kituyo.

Pia kwa upande wa mabroka walio hudhuria kikao hiko waliweza kuwasilisha changamoto zao kwa Mh. Mavunde zinazowakabili katika shughuli zao za uchimbaji wa madini ikiwemo ukosefu wa umeme katika vituo, pesa kutopatikana kwa wakati, ukosefu wa elimu ya madini hasa kwa wachimbaji wadogo, uchakavu wa mashine za uchimbaji, gharama za leseni kwa mabroka pamoja wakiomba serikali kurudisha soko la Tanzanite Mkoani Arusha.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: