Na John Walter-Manyara

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amefungua Maonesho ya Biashara Manyara yaliyoandaliwa na chemba ya wafanyabishara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA) ambayo yanafanyika eneo la stendi ya zamani Mjini Babati.

Kigahe amefungua maonesho hayo ya siku tano yanayojulikana kama (Tanzanite Manyara trade fair)leo Oktoba 18,2023 ,ambapo amewataka wafanyabiashara, wajasiriamali  kutumia maonesho hayo kubadilishana uzoefu ili kuboresha bidhaa zao.

Kigahe amezitaka  maonesho hayo pia yanayoa fursa kwa wafanyabishara, wajasiriamali na makampuni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki kuonyesha bidhaa zake, kujitangaza na kukuza soko la biashara kupitia soko huru la Afrika Mashariki.

Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Manyara Mussa Msuya, amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara Maeneo mbalimbali nchini kutangaza biashara zao na kupata masoko mapya. 

Hata hivyo Msuya ameomba Serikali kupitia Halmashauri kushirikiana na TCCIA katika uandaaji wa Maonesho hayo ili yaweze kufana zaidi.

Katika maonesho hayo, pia wadau kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi zimetumia fursa hiyo kuonesha bidhaa zao na kutoa elimu.

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema Halmashauri hazijatokeza kushiriki kwa sababu zilikuwa bize na Shughuli za kilele cha Mwenge wa Uhuru ambazo zilifanyika mkoani hapa Oktoba 14.

Maonesho hayo yalioandaliwa na TCCIA mkoa wa Manyara yamedhaminiwa na Kampuni ya Mati super Brands Ltd kupitia Kinywaji chake Cha Tanzanite premium Vodka.

Share To:

Post A Comment: