Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu, Dkt Dorothy Gwajima, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha siku ya Mwanamke anayeishi Kijiji Duniani itakayoadhimishwa Kijiji cha Olevolos kata ya Kimnyaki, Wilayani Arumeru Oktoba 15  2023.

Hayo yanesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha,Blandina Nkini wakati akifungua mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jukwaa la Mwanawake Kijijini yaliyofanyika kwenye uwanja wa Kijiji cha Olevolosi kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru

Aidha amesisitiza jamii kuzingatia maadili Ili kuondoa mmomonyoko wa maadili ambao kwa sasa limekuwa ni tishio kubwa kwa wananchi wa vijijini na mijini.

Amesema chanzo cha mmomonyoko wa maadili  ni familia kuyumba na kushindwa kutimiza wajibu na hivyo kusababisha mmomonyoko wa maadili.

Ameongeza kuwa wanawake ndio wazalishaji wakubwa lakini wamekuwa wakikandamizwa Kwa kunyimwa hali ya kumiliki mali na kushirikisha kwenye maamuzi.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha,Denis Mgie,amesema kuwa Kijiji hicho kimeweka Sheria mbalimbali ili kudhibiti changamoto zinazojitokeza katika malezi na hivyo kuwa Wakala mkubwa wa mabadiliko katika malezi na makuzi ya watoto nchini.

“Jamii inatakiwa kuongoza Kwa misingi mizuri kwa kuweka misingi ya watoto na Vijana Ili kuelewa nafasi ya mzazi au mlezi “ Amesema

Ameongeza kuwa  mmomonyoko wa maadili unachangiwa na baadhi ya wazazi au walezi kutokuwajibika kulea watoto kwa kuacha jukumu hilo kwa dada wa kazi na matokeo yake mtoto akiwa mkubwa anampeleka mzazi kwenye Kituo cha kulea wazee.

Kauli mbiu ya madhimisho hayo ni  Wezesha Wanawake wanaoishi Kijijini kwa uhakika wa chakula , lishe na  uendelevu kwa familia .


Share To:

Post A Comment: