Na John Walter-Manyara

Benki ya CRDB Tawi la Manyara imeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, huku wakiahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi.

Maadhimisho yao ambayo yamefanyika leo Oktoba 2,2023 katika ukumbi wa benki hiyo  na yatakwenda hadi Oktoba 6.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange,  amesema benki hiyo imeisaidia serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu.

Aidha amewapongeza watumishi wa CRDB kwa kufanya kazi kwa weledi,bidii, ubunifu na kutoa huduma stahiki kwa wateja wake akiwataka waendelee hivyo.

 Meneja Tawi la Benki ya CRDB Manyara Gloria Sam, amewashukuru wateja kwa kuendelea kuiamini benki hiyo, huku akiahidi wataendelea na utoaji wa huduma bora zaidi.


Share To:

Post A Comment: