WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ameujia juu uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutumia gari la wagonjwa kwa shughuli zingine. 


Badala yake, ameutaka uongozi huo kutumia gari hilo la Kituo cha Afya Rudi kwa lengo lililokusudiwa ili kusaidia kupunguza vifo vya wajawazito na wagonjwa wengine pindi linapohitajika.


Amesema ni aibu kuona gari la kubebea wagonjwa likitumika kwa ajili ya kufanyia mambo mengine huku kusudio la msingi likiwa limeachwa huku wajawazito na wagonjwa wengine mahututi wakihatarisha maisha yao. 


Simbachawene alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Rudi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi ya Chilendu, Jimbo la Kibakwe, Mpwapwa mkoani Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kimkakati ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

Share To:

Post A Comment: