Na Mwandishi wetu -Geita

Wadau mbalimbali wameeleza kuvutiwa na kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania kinachopatikana katika Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) lililopo kwenye maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa  Septemba 22,2023 na Meneja Masoko wa GST wakati akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa GST, amesema kuwa kitabu hicho ni toleo jipya ambalo limetoka mwaka 2023 likiwa na taarifa mbalimbali zinazoonesha madini yanayopatikana nchini Tanzania kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji. 

Priscuss amefafanua kuwa toleo hili ni tofauti na toleo la zamani, hii ni kutokana na toleo hilo jipya kuwa na taarifa nyingi zaidi za uwepo wa madini(occurrences) na pia linaelezea jiolojia ya mkoa husika pamoja na ramani yake.

Akizungumzia kuhusu uwepo wa kitabu hicho ,Priscus ametumia fursa hiyo kuwaalika wadau wote wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini kutumia kitabu hicho sambamba na taarifa nyingine za jiosayansi utafiti wa jiosayansi ili kuongeza tija katika shughuli za utafutaji na uchimbaji madini.


Sambamba na kitabu hicho GST katika maonesho hayo imekuja na machapisho mbalimbali ya jiosayansi yanayoelezea jiolojia na aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini Tanzania.

Aidha , akielezea kuhusu uchunguzi wa madini maabara, ametoa wito kwa wadau kutumia maabara ya madini ya GST kwani ni ya kisasa na majibu yake ni ya uhakika. Pia, amewaalika wadau wenye changamoto za kujua miamba au madini waliyonayo kufika katika banda hilo na kupima bure ili watambue aina ya miamba na madini waliyonayo.

Maonesho ya Teknolojia ya madini kwa mwaka 2023 yanabebwa na kaulimbiu inayosema *"Matumizi sahihi ya Teknolojia katika kuinua Wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira*
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: