Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri wa nchi - Utumishi na Utawala Bora amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jukwaa la Wazalendo Huru ofisini kwake Chalinze.

Ujumbe huo wa viongozi wa taasisi hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti Bi. Khadija Juma walimshukuru Mbunge kwa kutenga muda kuwaona na pia kueleza nia yao ya kuhitaji kufanya kazi katika halmashauri ya Chalinze hasa kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo na kupambana na uharibifu wa maadili katika jamii yetu. Pamoja na hayo, Mwenyekiti wa taasisi Bi. Khadija alimuomba Mbunge kukubali kuwa mlezi wa taasisi yangu , jambo ambalo Lilikubaliwa.  

Kwa upande wa Mbunge, aliwashukuru vijana hao kwa kuanzisha taasisi hiyo nanmalengo ambayo ameyaita kuwa “malengo ya kukomboa jamii yetu.”  Akizungumza na viongozi wa Taasisi hiyo, aliwaomba kuendelea kusimamia malengo yao na kuwakaribisha sana Chalinze wafanye kazi kuhamasisha maendeleo. #KaziInaendelea #Chalinze

Share To:

Post A Comment: