Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Bw. Vedastus Mwita akizungumza na waandishi wakati wa kongamano hilo na kueleza kuwa Shirika hilo linaendelea kufanya maboresho makubwa katika utoaji wa huduma hususani katika miundombinu ya Mawasiliano ya simu kupitia mkongo wa Taifa. Leo visiwani Zanzibar.

 SHIRIKA La Mawasilisho Tanzania (TTCL) likiwa kitovu cha Mawasiliano limeendelea kuhakikisha huduma ya intaneti inapatikana katika kiwango cha juu katika kongamano la Kimataifa la kujadili fursa za kiteknolojia kwa kuwawezesha washiriki na wadau wa mkutano huo kutumia huduma za mtandao wa TTCL kuperuzi kwa uharaka na urahisi zaidi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo visiwani Zanzibar katika kongamano la kimataifa la kujadili fursa za kiteknolojia, (Connect 2 Connect,) Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Bw.Vedastus Mwita amesema huduma ya intaneti imefanikiwa kutokana na uwepo wa miundombinu imara inayowekwa na Shirika hilo

"TTCL si tu kama mtoa huduma za mawasiliano ya simu bali kama mhusika mkuu aliyepewa mamlaka ya kupanga, kujenga, kuendesha na kudumisha miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano ya simu, ambayo inaweza kubadilika kulingana na mabadiliko ya kisasa ya kiteknolojia na miundombinu hiyo imeundwa ili kuendana na mwingiliano wa waendeshaji ndani na nje ya Tanzania." Amesema.

Aidha amesema, kwa sasa TTCL imefanya mabadiliko makubwa katika kuboresha utoaji wa huduma ambapo imehakikisha miundombinu ya Mawasiliano ya simu kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) umeboreshwa ambapo kwa sasa unapakana na nchi 8.

Mwita amesema, TTCL inahakikisha uhifadhi data kwa kutoa suluhisho na vifaa vya kutunza Data kwa kupitia kituo cha kutunza data Kimtandao (NIDC) kilichoidhinishwa na ISO.

Vilevile amesema, TTCL inahakikisha inakuwa ndio lango la huduma za E-serikali kwa kukaribisha miundombinu na huduma muhimu za Tehama pamoja na lango la usalama la kitaifa kielektroniki kwa kuimarisha usalama wa sekta ya mawasiliano.

Kongamano hilo la siku mbili (06-07 Septemba 2023) lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Madinat Al Bahr visiwani Zanzibar limewakutanisha wadau zaidi ya 250 wa Tehama na kujadili ukuaji wa Teknolojia, fursa mbalimbali za kibiashara pamoja na ushirikano wa kibiashara.


Matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo.

Share To:

Post A Comment: