Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi, Jones Olotu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) akitoa taarifa ya mkoa wa Mtwara kuhusu usambazaji wa umeme vijijini mbele Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (Aliyekaa mbele) kushoto kwake na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishaji Vijiji (REA) Mama Janet Mbene mapema leo katika ofisi za TANESCO Mtwara.

 Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi, Jones Olotu amemweleza Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ambaye ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishaji Vijiji (REB) Mama Janet Mbene kuwa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekamilisha na kuendeleza miradi mbalimbali ya kusambaza nishati ya umeme mkoa wa Mtwara na kwamba fedha hizo zimechangia katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwa Wananchi wa mkoa wa Mtwara ambao wengi wao wanaishi vijijini.


Akitoa taarifa hiyo leo, Tarehe 15 Septemba, 2023 kabla ya kuanza kwa ziara ya Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mtwara,

Kiasi hicho cha fedha, kimetumika kutekeleza Miradi mbalimbali mkoani humo; Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili, Mradi wa kusambaza umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo, Mradi wa kusambaza umeme kwenye vituo vya afya na visima vya maji ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko, ukiwemo UVIKO 19 pamoja na Mradi wa kusambaza umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji Awamu ya Tatu (Peri Urban III).

Akieleza kuhusu historia fupi ya upatikanaji wa umeme kwenye vijiji vya mkoa wa Mtwara, Mhandisi Olotu amesema mkoa wa Mtwara una jumla ya vijiji 785, ambapo hadi kufikia tarehe 10 Septemba, 2023 jumla ya Vijiji 540 vimeshaunganishwa na umeme kupitia miradi mbalimbali; na Vijiji 345 vitapatiwa umeme kupitia mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili, unaotekelezwa na Wakandarasi wawili ambao ni kampuni ya Central Electricals International Ltd, inayojenga Fungu 20 (Lot 20) ambaye anatekeleza mradi katika Wilaya za Mtwara, Tandahimba na Newala kwa gharama ya shilingi bilioni 61.63.

Mkandarasi kampuni ya Namis Corporate Ltd (Lot 19) ambaye atetekeleza mradi katika Wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa gharama ya shilingi bilioni 35.60. Jumla ya gharama za Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili kwa mkoa wa Mtwara unagharimu shilingi bilioni 97.23.

Mhandisi Olotu ameongeza kuwa ili kufikia lengo la Serikali kufikisha umeme katika vijiji vyote, Wakala uliongeza kazi kwa Wakandarasi katika vijiji 112 ambavyo havikua vimejumuishwa katika wigo wa awali na hivyo kufikia jumla ya vijiji 276 katika wigo wa kazi.

“Kutokana na uhitaji mkubwa wa kuwafikia Wateja wengi zaidi, Wakala uliongeza km 2 za umeme wa msongo mdogo na wateja 42 kila kijiji kwa jumla ya vijiji 276 vijivyopo katika fungu/Lot 20 la Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili”. Alisema, Mhandisi Olotu.

Mhandisi Olotu, amemalizia kuwa, kwa ujumla utekelezaji wa Miradi hiyo yote kwa mkoa wa Mtwara una wastani wa asilimia 60.

Naibu Waziri wa Nishati pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) wapo mkoani Mtwara kwa ajili ya kushiriki kwenye ziara ya Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ameanza ziara ya kiserikali katika mkoa wa Mtwara, kuanzia leo jioni Tarehe 15 hadi 17 Septemba, 2023 ambapo anatarajiwa kukagua na kuzindua Miradi mbalimbali ya maendeleo, kupitia Sekta ya Afya, Kilimo, Uchukuni/Usafirishaji pamoja na Nishati.

Viongozi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakufuatilia mkutano huo wa Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishaji Vijijini (REB); Mama Janet Mbene akisaini kitabu cha wageni mapema leo kabla ya kuanza mkutano na huo katika ofisi za TANESCO Mtwara.
Mhandisi, Innocent Luoga, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati akitoa taarifa ya jumla kuhusu maendeleo ya Sekta ya Nishati mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga.
Share To:

Post A Comment: