Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) imezinduliwa leo Jumatano Septemba 20,2023 Mkoani Shinyanga huku waratibu wakiagizwa kuandaa mpango kazi utakaogusa maeneo yote ya kimkakati.

Programu hiyo inatekelezwa katika Mikoa 26 ya Tanzania bara ambapo uzinduzi kwa ngazi ya Taifa ulifanyika Desemba 13,2021 ambapo ilizinduliwa na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maaluma Dkt. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizindua programu hiyo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewaagiza waratibu wa PJT – MMMAM kufanyakazi kwa ubunifu na kuandaa mpango kazi unaogusa maeneo yote ya kimkakati ikiwemo kuzifikia sekta za umma na sekta binafsi.

DC Mkude amewaomba wadau na watu wote watakaoshiriki kwenye PJT – MMMAM kuhakikisha wanatoa kipaumbele na kuweka mipango ya utekelezaji wa maeneo hayo kuanzia ngazi ya familia na maeneo ya kazi.

“Nawaagiza waratibu kufanyakazi kama timu ya ushindi kwa kuandaa mpango kazi unaogusa maeneo yote ya kimkakati na kuzifikia sekta za umma na sekta binafsi lengo ni kuwapa fursa waajiri na watumishi wao ili kuhakikisha wanatoa fursa na kipaumbele katika malezi, makuzi na malezi ya awali ya mtoto wakati wawapo kazini na nyumbani”.amesema DC Mkude

Awali akizungumza afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale amesema utekelezaji wa programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) umelenga maeneo makuu matano (5) ya kimkakati ambayo ni pamoja na upatikanaji wa Afya bora kwa mtoto, lishe bora kwa mtoto, malezi ya mwitikio, usalama na ulizi wa mtoto pamoja na fursa za ujifunzaji wa awali.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la ICS Sabrina Majikata amesema PJT – MMMAM imelenga kuwaimarisha watoto kuanzia umri 0 hadi miaka nane (8) ambapo amesema ni jukumu la kila mtu kuwalinda watoto wa kike na watoto wa kiume ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao.

Baadhi ya viongozi wa serikali na wadau akiwemo katibu wa kampeni ya kupinga ukatili inayoitwa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga,  Bwana Daniel Kapaya amesema programu PJT – MMMAM itasaidia kupunguza ukatili unaoendelea katika jamii.

Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) imezinduliwa leo Jumatano Septemba 20,2023 Mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, taasisi binafsi pamoja na wadau mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizindua Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo Septemba 20,2023.

Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga leo Jumatano Septemba 20,2023.

Mwakilishi kutoka shirika la ICS Sabrina Majikata amesema PJT – MMMAM akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga leo Jumatano Septemba 20,2023.

Mwakilishi kutoka TECPEN akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga leo Jumatano Septemba 20,2023.

Ngasa Michael akizungumza kwa niaba ya menaja  World Vision kanda ya ziwa leo Jumatano Septemba 20,2023 kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga.

Mwakilishi kutoka shirika la Doctors with Africa (CVAMM), Chiara Didone akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga leo Jumatano Septemba 20,2023.

Meneja wa NMB Manonga Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Gadiel Sawe akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga leo Jumatano Septemba 20,2023.

Katibu wa kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoani Shinyanga leo Jumatano Septemba 20,2023.

Hafla ya uzinduzi wa programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ikiendelea leo Septemba 20,2023 katika ukumbi wa Vigimark Manispaa ya Shinyanga.



Share To:

Misalaba

Post A Comment: