Na John Walter-Manyara

Takwimu za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) zinaonyesha kuwa zaidi ya watoto milioni nne wanaoishi na kufanya kazi  mitaani zaidi ya asilimia 40 wametoka kwenye familia zilizovunjika.

Akizungumza katika kikao cha Maafisa ustawi wa Jamii wa kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara jijini Dodoma, Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC)  Anna Henga amesema wamekuwa wakitatua migogoro  mingi ya ndoa ambapo waathiriwa ni watoto zaidi.

Amesema ni faraja kubwa kwao kushirikiana na serikali katika ulinzi wa haki za binadamu.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan  anaonyesha ni ya dhati ya kuhakkisha anatetea haki za wanawake na watoto na kuweka maslahi kwa maafisa ustawi wa jamii.

Share To:

Post A Comment: