Viongozi mbalimbali wa Chama Cha RUNALI pamoja viongozi mbalimbali wa kisiasa walishiriki zoezi la utoaji wa msaada wa baiskeli Kwa mkulima huyo
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha RUNALI pamoja viongozi mbalimbali wa kisiasa walishiriki zoezi la utoaji wa msaada wa baiskeli Kwa mkulima huyo


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


CHAMA kikuu cha ushirika cha Ruangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI) mkoani Lindi kimemekabidhi baiskel moja kwa mkulima anaeitwa Ismail Issa Chitanda (Nduli) ambae ni mlemavu wa miguu yenye thamani ya zaidi ya milioni moja Kwa lengo la kumsaidia katika shughuli za Kila siku.

Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hiyo, Meneja wa chama cha RUNALI Jahida Hassan alisema kuwa wamenunua baiskeli hiyo kutokana na makato ya wakulima baada ya kuuza mazao kwenye chama hiyo.

Hassan alisema kuwa chama cha RUNALI kimekuwa kikitenga mara Kwa mara fedha Kwa ajili ya kurudisha kwa jamii ilikiwa ni kutoa msaada Kwa jamii ya watu wenye uhitaji wa jambo Fulani.

Alisema kuwa kurudisha huduma kwa jamii (CSR) limekuwa jambo jema ambalo limekuwa likitoa faraja Kwa watu wenye uhitaji wa jambo Fulani na kusaidia watu hao kuendelea na kilimo Cha mazao mbalimbali.

Kwa upande wake mkulima huyo Ismail Issa Chitanda alisema kuwa anakishukuru chama cha RUNALI Kwa msaada wa baiskeli hiyo kuwa utamsaidia katika shughuli za kiuchumi hasa kilimo ambacho amekuwa analima mara Kwa mara.

Chitanda alisema kuwa ataitunza baiskeli hiyo ili iweze kudumu Kwa miaka mingi na kuwa mfano kwa watu wengine ambao hupewa msaada huo.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: