Na John Walter-Manyara    

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, amewapongeza viongozi na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jimbo la  Mbulu kwa ujenzi wa kitega Uchumi kikubwa na cha kimkakati, kitakacho chochea huduma, biashara na ajira katika wilaya ya Mbulu.                         

Komred Kheri James ameyasema hayo mapema leo katika ibada ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi na Harambee ya ukamilishaji wa jengo hilo la kitegauchumi, ilio ongozwa na Mkuu wa KKKT Mteule Baba Askofu Dkt.Alex Malasusa ambae pia ni Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.                                      

Akiwasilisha salamu za Serikali, Komred Kheri James ameeleza kuwa mahusiano ya Serikali na madhehebu ya Dini wilayani humo ni mazuri na yamekuwa ni Msingi wa ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya, usimamizi wa maadili na vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.             

Kupitia Harambee hiyo ambayo ilijumuisha Wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo Komred Kheri James amekabidhi kiasi cha shilingi 12,500,000/= Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni mchango wake wa kuunga mkono uwekezaji huo mkubwa utakao kuwa kuchochea cha maendeleo na Uchumi wa Mji wa Mbulu.     

Akizungumza baada ya Harambee hiyo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mbulu Baba Askofu Nicholas Nsangenzelu amewashukuru Wananchi na watumishi wote na kipekee Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono uwekezaji huo muhimu kwa kuchangia pamoja na Wananchi wengine.

Share To:

Post A Comment: