Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya wasichana mkoank Mtwara, ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya vipaji vya Sayansi.
Mhe. Dkt. Samia ameeleza hayo leo Septemba 16, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa halmashauri ya Mji Nanyamba, wakati akiwa njiani kuelekea wilayani Tandahimba ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Mtwara.
Dkt. Samia amesema ujenzi wa shule hiyo ni muendelezo wa Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kuwa inawekeza katika elimu kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari - (Sequip) ili kuzalisha madaktari, wahandisi na wataalam wengine wa kike ambao watakuja kushika nafasi mbalimbali miaka ijayo.
“Tunataka watoto wa kike wa Mtwara hususani ni Nanyamba wasome wawe wanasayansi tuchunge wasichana Wetu, Kina Samia watatoka huku huku Nanyamba ila msipowalinda wasichana hao watatoka katika maeneo mengine na lengo la nyie kujikomboa kupitoa elimu halitafanikiwa’ ameeleza Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
Aidha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka wakazi wa Mtwara kuwaacha watoto wakike watimize ndoto zao kielimu, wakati Serikali ikiendelea kuwajengea misingi bora ya kupata elimu.
“Lakini mkianza kuwashughulikia mapema hivi mnavyofanya, hawa wasichana hawatafika kule, shule tunayojenga haitakuwa na wasichana haitakuwa na watoto na wakiwepo watatoka mkoa mwingine kuja huku kwenu.”
“Nawaomba sana kina mama, kina mama baada ya mavuno mambo ya kuwacheza wasichana na kuwaambia sasa mpo huru nendeni yasiwepo, tuchunge wasichana wetu wakina Samia watatoka huku Nanyamba, mkiwashughulikia mapema hawa hawatakuja juu.” Dkt. Samia.
Mhe. Rais Skt. Samia Suluhu Hassan yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku nne itakayohitimisha Septem
Post A Comment: