Mkuu wa wilaya ya Longido Marko Henry Ng'umbi amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Billioni tatu kwaajili ya ujenzi wa shule kubwa ya sayansi ya wasichana inayojengwa Katika Kata ya Oribomba wilaya Longido  mkoani  Arusha.

Akizungumza nasi mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa wameanza ujenzi huo kwa zaidi ya wiki sasa ambapo kwa majengo yote ya shule hiyo wamefikia hatua ya uchimbaji wa msingi na kusogeza vifaa vyote vya ujenzi wa majengo hayo.

"Tunategemea kuanzia wiki ijayo majengo yote yatakuwa yamefikia katika hatua za kuta matarajio yetu ni kwamba mradi huu ifikapo Disemba 31 majengo yote yatakuwa yamekamilika na mwezi Januari wanafunzia wataanza masomo ya rasmi."alisema.

Hata hivyo Dc Ngumbi alisema wanapata ushirikiano mzuri kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na kamati zinazosimamia ujenzi kutokana na ujenzi wa shule hiyo kujengwa kwa mfumo wa "Force account" ,ambapo kila majengo yamepata fundi,sisi kama Serikali kazi yetu ni kuhakikisha tunasimamia   thamani ya fedha na thamani ya ubora wa mradi.

Ikumbukwe kupitia mradi huu wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) wa miaka mitano, Serikali imetenga Shilingi Trilioni 1.2 ambazo zinajenga shule mpya za Sekondari 1,026 kati ya hizo shule 26 ni shule Maalum za wasichana zinazojengwa moja kila mkoa.

Kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari kila mkoa unapewa bilioni 4 kwa awamu mbili kujenga shule ya wasichana ya bweni ambayo itakuwa na Uwezo wa kupokea wanafunzi 1,080 na kidato cha kwanza hadi cha sita”
Share To:

Post A Comment: